Posted by Esta Malibiche on JAN 11,2017 in NEWS
Mbunge
wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi kulia akisikiliza kilio cha
wafanyakazi wa zahanati na vituo vya afya alipotembelea kujionea na
kusikiliza changamoto za huduma za afya katika jimbo lake ili
kuzitafutia ufumbuvi na kuboresha huduma hiyo.
Na fredy mgunda,Iringa
MBUNGE
wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi alifanya ziara ya kuzitembelea
zahati,vituo vya afya na hospitali za jimbo hilo kwa lengo la kujionea
changamoto za kiafya.
Akiwa
katika ziara hiyo alikumbana na changamoto ya kukosekana kwa umeme
katika baadhi zahati za jimbo hilo na kuahidi kulipeleka tatizo hilo
bungeni ili litafutiwe ufumbuzi mapema.
Akizungumza
na blog hii Chumi alisema tatizo la umeme katika vituo na zahati ni
kubwa hivyo inahitajika nguvu ya ziada kutatua tatizo la umeme ili
kuboresha afya za wananchi wake pamoja na huduma ya mama na mtoto.
“Hii
inasikitisha sana hebu angalia zahati zinavifaa vyote mhimu ila umeme
ndio tatizo hatuwezi kupata huduma bora kama hakutakuwa na umeme
tunaelekea bungeni nitaenda kuongea na waziri husika ili kutatua
changamoto hii” alisema Chumi
Aidha
mh chumi alisema kuwa anapenda kuhakikisha kuwa umeme wa REA awamu ya
tatu unazifikia zahati zote pamoja na vijiji husika kwa kuwa serikali
inalengo la kusambaza umeme vijiji vyote nchi nzima hivyo hata vijiji
vya jimbo la Mafinga Mjini vimo katika mpango huo.
Nao
baadhi ya Wananchi walimpongeza mbunge huyo kwa kazi kubwa anayoifanya
kuwaletea maendeleo katika jimbo la Mafinga Mjini ndani ya mwaka mmoja
tu amefanya vitu vingi vizuri tofauti na matarajio ya watu wengi.
“Angalie
nyie waandishi wa habari Mbunge Cosato Chumi kwa mwaka moja tu
ametengeneza barabara karibi a zote za jimbo huku nyingine zikiwekwa
rami,amehangaikia swala la maji tunaona matumaini,swala afya ndio
kafanya vitu vingi,michezo ndio mechi zinaendelea na mambo mengine mengi
huyu mbunge ni wakuigwa kwa juhudi zake” walisema wananchi
Wananchi
hao waliongeza kuwa swala la umeme mbunge wetu ametueleza vizuri sana
hivyo tunaimani ya maneno na vitendo yake kuwa analishughurikia kwa
umuhimu mkubwa.
Baadhi
ya madiwani wa jimbo hilo walisema kuwa kuwa mbunge huyo amekuwa
akiwasaidia kutatua changamoto nyingi za kitendaji na kuifanya kazi yetu
ya udiwani kuwa rahisi kutokana na mambomengi anayafanya mbunge wetu
Cosatio chumi.
“Tunamshukuru
Mbunge wetu kwa kuwasaidia wananchi taa za sola kwa vijiji ambavyo
havina umeme hizo ni juhudi zake binafsi na sio hilo kafanya mambo mengi
sana hadi sasa tunajiona tupo kwenye halmashauri kongwe kumbe ni
halmashauri mpya” walisema baadhi ya wadiwani
Kwa
upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Charle Makoga
amesema kuwa changamoto ya umeme ni kubwa katika vijiji ambavyo
havipokupata umeme wa REA awamu ya kwanza na pili na ndio sababu
inayosababisha huduma za kiafya kudorola katika baadhi ya vijiji.
0 maoni:
Chapisha Maoni