Posted by Esta Malibiche on JAN 17,2017 IN NEWS
Kaimu
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (kulia)
akielekea katika Gati namba moja la Bandari ya Tanga kuangalia shughuli
mbalimbali zinazoendelea bandarini hapo. Penmbeni yake ni Mhandisi wa
Bandari hiyo Bw. Saleh Sapi.
Na Adili Mhina, Tanga.
Mamlaka
ya Bandari nchini imeshauriwa kuangalia taratibu za kurasimisha bandari
bubu ili kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali pamoja na kuhakikisha
bidhaa zinazopitishwa katika maeneo hayo zinakubalika kisheria.
Ushauri
huo umetolewa hivi karibuni na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya
Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati timu ya ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Tume ya Mipango ilipofanya ziara katika Bandari ya
Tanga kwa lengo la kufanya ufuatiliaji na tahmnini ya shughuli
zinazotekelezwa bandarini hapo.
Mwanri
alieleza umuhimu wa kurasimisha bandari bubu baada ya kupata taarifa
kuwa katika Mkoa wa Tanga pekee kuna bandari bubu takriban 42 ambazo
zinaendesha shughuli mbalimbali bila ya usimamizi wa Mamlaka ya
Bandari.
Mhandisi
wa Bandari ya Tanga Bw. Saleh Sapi (mwenye t-shirt) akitoa maelezo kwa
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (koti
jekundu) juu ya kina cha maji katika bandari hiyo. Upande wa kulia ni
Bw. Jordan Matonya na Bi Anna Kimwela, wachumi kutoka Tume ya Mipango.
Upande wa kushoto (mwenye miwani ya jua) ni Afisa Mipango Mwandamizi wa
Bandari ya Tanga, Bibi Moshi Mtambalike.
Mwanri
alieleza kuwa kwa sasa Serikali haiwezi kuendelea kufumbia macho suala
hilo kwani licha ya Serikali kupoteza mapato yake wapo baadhi ya watu
wanaotumia njia hizo nyakati za usiku kuendesha shughuli zinazoenda
kinyume na kisheria na taratibu za nchi, hivyo kuchochea uhalifu.
“Kuna
umuhimu mkubwa kuangalia shughuli zinazoendelea katika bandari bubu kwa
kuwa wakati mwingine wafanya biashara wanaopaswa kulipa kodi wanatumia
maeneo hayo kupitisha bidhaa bila kulipa kodi na wengine wanatumia
bandari bubu kuendesha biashara haramu. Ni lazima kuanza kufanya
utaratibu wa kurasimisha bandari hizo ili kuharakisha maendeleo ya nchi
yetu,” alisema Mwanri.
Pamoja
na hayo, Mwari alitembelea maeneo ya Bandari ya Tanga na kushuhudia
shughuli mbalimbali zikiendelea ikiwa ni pamoja na ujenzi wa gati namba 2
ikiwa ni moja ya malengo katika kuimarisha huduma za upakiaji na
upakuaji wa mizigo bandarini hapo.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akikagua ukarabati wa boti katika Bandari ya Tanga.
Awali,
Mhandasi wa Bandari hiyo Bw. Saleh Sapi alieleza kuwa Bandari ya Tanga
inapokea tani laki mbili za mizigo kwa mwezi ambapo bidhaa kubwa
zinazoingizwa kutoka nje ni malighafi ya kutengenezea saruji wakati
bidhaa zinazosafirishwa kwenda nje ni kahawa, mkonge, pamoja na mbao
ambazo kwa sasa kibali chake kimesitishwa kwa muda.
Mhandisi
huyo alieleza kuwa Bandari ya Tanga haina eneo lenye ukubwa wa kutosha
kwa ajili ya kutekeleza huduma zake kwa ufanisi huku kina cha maji
kikiwa ni mita nne kitu kinachopelekea meli kubwa kushindwa kufika
kwenye gati za bandari na badala yake matishari hutumika kubeba mizigo
hiyo.
Mhandisi
Sapi alifafanua kuwa kutokana na changamoto hiyo nguvu kubwa
inaelekezwa katika kuangalia namna ya kujenga bandari kubwa ya kisasa
katika eneo la Mwambani ambapo kuna kina cha maji kinatosha kuhudumia
meli kubwa na pia kuna eneo la kutosha shughuli mbalimbali za bandarini.
Shughuli za kupakia Magogo ya Umeme zikiendelea katika Bandari ya Tanga.
Mhandisi
wa bandari ya Tanga Bw. Saleh Sapi akimueonesha Kaimu Katibu Mtendaji
wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri ujenzi unaoendelea (hauonekani
pichani) wa gati namba mbili katika Bandari ya Tanga. Pembeni ya
Mhandisi Sapi ni Mchumi Mkuu kutoka Tume ya Mipango Bw. Aloyce Shayo na
wa kwanza kulia ni Bw. Jordan Matonya Kutoka Tume ya Mipango.
Ujenzi wa gati namba mbili ukiendelea katika Bandari ya Tanga.
PICHA ZOTE NA ADILI MHINA, TUME YA MIPANGO.
0 maoni:
Chapisha Maoni