Jumatatu, 2 Januari 2017

​DC MUFINDI AFANYA ZIARA KIWANDA CHA CHAI KUFUATIA TISHIO LA KUFUNGWA KWA KIWANDA HICHO

 Posted by Esta Malibiche on JAN 2,2017 in NEWS

 Meneja wa kiwanda akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya

Mmoja wa  Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalam wilaya ya Mufindi akifafanua jambo ndani ya kiwanda hicho
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalam wilaya ya Mufindi wakimsikiliza kwa makini mameneja wa kiwanda hicho




Mkuu wa Wilaya ya Mufindi JAMHURI WILLIAM amefanya ziara katika kiwanda cha chai MTC kilichopo kijiji cha ITONA Halmshauri ya Wilaya ya Mufundi baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa mwekezaji wa kiwanda hicho anakusudia kukifunga.


Mkuu wa Wilaya ameamua kufanya ziara kiwandani hapo akiwa na kamati yake ya ulinzi na usalama ya Wilaya ili  kuzungumzo na mwekezaji huyo ajue tatizo nini mpaka afikirie kufunga kiwanda na kuhatarisha maisha ya watu wa Mufindi ambao wanaendesha maisha yao kwa kutegemea kiwanda hicho kwani kiwanda hicho pekee kimeajiri zaidi ya watu elfu 50.


Baada ya mazungumzo marefu, mwekezaji huyo alimhakikishia mkuu wa Wilaya kuwa kiwanda hicho hakitafungwa licha ya changamoto za kiuchumi anazozipitia ambazo zimesababisha tanesko wakate umeme kwa kuchelewa kulipa bili ya mwezi mmoja ya Zaidi ya shilingi milioni 100, kisha akamuomba Mkuu wa Wilaya asaidie baadhi ya changamoto zinazotokana na masuala ya kisera.


Halmshauri ya wilaya ya Mufindi inajumla ya makapuni makubwa matano (5) yaliyowekeza kwenye viwanda vya kuchakata chai kutokana na hali ya hewa rafiki kwa kilimo cha chai.

0 maoni:

Chapisha Maoni