Posted by Esta Malibiche on JAN28,2017 IN BURUDANI
Shindano
la kumsaka mlimbwende wa MISS KIBOSHO 2017 Jijini Mwanza limeanza jana
katika viunga vya Kibosho Luxury Bar iliyopo Kiseke Ilemela Jijini
Mwanza ambapo wanyange 10 wanawania nafasi hiyo.
Wanyange
hao kama wanavyoonekana pichani ni Caren Nestory, Dorice Ezra, Jullieth
Michael, Elizabeth Faustine, Christina Lucas, Nasra Ramadhan, Jacline
Moses, Denzry Michael, Kephlin Jacob na Aida Gazar.
Shindano
hilo limeandaliwa na Raj Entertainment kwa udhamini wa Kibosho Luxury
Bar, Wema Salon na Ngenda Salon huku likiwa limelenga kukuza sanaa ya
ulimbwende kuanzia za mitaa hadi kitaifa.
Baada
ya usiku ya kuamkia leo wanyange hao kuchuana vikali, fainali
itafanyika leo kuanzia majira ya saa moja jioni katika viunga hivyo vya
Kibosho Luxury Bar Kiseke Jijini Mwanza kwa kiingilio cha shilingi 5,000
tu.
Binagi Media Group
Wanyange wa shindano la Miss Kibosho 2017 wakionesha makeke yao jukwaani
Washereheshaji
wakimtambulisha Matron wa Miss Kibosho 2017, Fania Hassan (katikati)
ambaye alikuwa Miss Utalii nchini mwaka 2006.
Kila
mlimbwende alionesha makeke ya hali ya juu hadi kuwapa wakati mgumu
majaji. Kumbuka majaji ni Leonald Kaduguda (kushoto), Mama Ngenda Lutalo
(katikati) na Mwl.Tatu Ngelengela (kulia).
Umakini katika kufuatilia kinyang’anyiro cha Miss Kibosho 2017
Majaji
wakiahilisha shindano la Miss Kibosho 2017 usiku wa kuamkia leo.
Kushoto ni Leonald Kaduguda, Mama Ngenda Lutalo (kulia) na Mwl.Tatu
Ngelengela (katikati). Fainali itafanyika leo jioni kuanzia majira ya
saa moja kamili.
0 maoni:
Chapisha Maoni