Mazoezi mpira wa Netball yakiendelea
…………………………………………………………………………………………………………
Mwandishi Wetu
TIMU ya netiboli ya Uchukuzi SC
iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kesho
itarusha karata yake ya kwanza kwa kuumana na wenyeji CDA Dodoma katika
mchezo wa netiboli, utakaofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri.
Uchukuzi SC iliyoundwa na
wachezaji mahiri imekuwa katika mazoezi ya muda mrefu, huku ikipata
mechi kadhaa za kirafiki dhidi ya timu maarufu ya Cargo na Uhamiaji zote
za jijini Dar es Salaam.
Kocha Mkuu wa timu hiyo, ambaye
pia ni mchezaji wa zamani wa Bandari na timu ya Taifa, Judith Ilunda
alisema wamekuja kushindana na sio kuwa wasindikizaji, ambapo
wanatarajia ushindi mnono dhidi ya wapinzani wao.
Hatahivyo, Ilunda alisema CDA sio
timu ya kubeza kwani inaundwa na wachezaji wazoefu, wenye kujua mbinu
mbalimbali za uchezaji, hivyo atahakikisha wachezaji wake watacheza kwa
tahadhari, ili kuibuka na ushindi.
“Tumekuja kushindana huku na
kamwe hatutakubali kuwa wasindikizaji, hivyo nitahakikisha wachezaji
wangu wanajituma kila idara ili tushinde kwani hii timu tunayocheza nayo
inawachezaji wakongwe na wenye uzoefu,” alisema Ilunda.
Aliwataja wachezaji wanaounda
kikosi mahiri na nafasi zao uwanjani kuwa ni Matalena Mhagama (GA),
Subira Jumanne (WD), Mwadawa Hamis (GD), Sharifa Mustafa (GK), Mary
Kajigiri (WA) na Mayasa Hamidu .
Wachezaji wengine ni Grace
Mwasote (GS), Neema Makassy (WD), Johari William (GK), Salama Mbuguni
(WA), Mwanaisha Athuman (WD) na Tatu Kitula (GS).
Timu hiyo mwaja jana katika
mashindano ya Mei Mosi iliyofanyika Mwanza ilishika nafasi ya pili,
baada ya kukutana na Utumishi katika fainali.
Michezo hii ya Mei Mosi, ambayo
ilianza jana (Jumanne) inazinduliwa rasmi leo (Jumatano) na mgeni rasmi
mkuu wa mkoa, Jordan Rugimbana.
0 maoni:
Chapisha Maoni