Ijumaa, 15 Aprili 2016

TAKUKURU MKOANI PWANI YAZITAJA TAASISI NA IDARA 11 ZINAZOONGOZA KWA MALALAMIKO YA VITENDO VYA RUSHWA


ki1
Kamanda wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzan Rymond  akiwaonyesha waandishi wa  habari ofisini kwake hawapo pichani orodha ya  majina ya taasisi na idara ambazo  zimeongoza kwa malalamiko ya vitendo vya rushwa (Picha na Victor Masangu)
ki2
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo wa Takukuru.
……………………………………………………………………………………………
 NA VICTOR MASANGU, PWANI
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoani Pwani imezitaja taasisi na idara zipatazo 11 ambazo zimelalamikiwa  kuhusika katika  matukio mbali mbali  ya vitendo vya kupokea rushwa kinyume kabisa na
sheria na taratibu za nchi.
Akizungumza katika mkutano na  waandishi wa habari ofisini kwake wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi januari hadi machi mwaka huu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzan Rymond  alisema  kuwa wale waliohusika watapeekwa katika vyombo vya sheria.
Susan alisema kwamba kwa sasa wamepokea jumla ya malalamiko 49 yanayohusina na vitendo vya rushwa  baada ya kufanya uchunguzi waa wa wameweza kubaini idara inayoongoza kwa malalaamiko hayo kwa Mkoa  mzima wa Pwani  ni  serikali za mitaa ambayo  ina jumla ya malalamiko 18.
Kamanda huyo alifafafnua kuwa idara  nyingine iliyoshika nafasi ya pili ilikuwa ni afya ambayo ilipata malalamiko 8,polisi 4,mahakama 3 ardhi 3 sekta binafsi 3 elimu 2 tanesco 2 fedha 1 vipimo 1 pamoja na maji 1.
“Ndugu zangu waandishi wa habari leo tumewaita ili kuwapa taarifa ua utekelezaji wa majukumu yetu kwa kipindi cha kuanzia mwezi januari hadi kufikia mwezi machi, na katika miezi hiyo tumepata malalamiko mengi yanayohusina na vitendo vya rushwa katika mkoa wetu wa Pwani.
Aidha Kamanda huyo alisema malalamiko ambayo wameshayapokea katika ofisi yaa ni 64 ambapo kati yao 49 ndio yanahusina na  malalamiko ya vitendo vya upokeajiwa  rushwa katika idara za serikali pamoja na taasisi mbali mbali.
Pia Suzan alisema kwamba kwa sasa katika kuhakikisha wanakomesha vitendo vya kupokea na kutoa rushwa wataendelea kufanya uchunguzi wa kina katika maeneo mbali mbali ili pindi watakapowabaini wahusika waweze kuwachukulia kali na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Kamanda huyo alisema hadi sasa tayari kuna jumla ya kesi  22 zinazohusiana na vitendo vya rushwa  ambazo zimeshafikishwa  mahakamani,na pia bado kuna baadhi ya kesi nyingine bado zinafanyiwa uchunguzi zaidi.
Katika hatua nyingine Kamanda huyu aliwaomba wananchi wote wa Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanatoa taarifa katika vyombo vinavyohusika endapo wakibaini kuna daily zoozte za mtu kutoa au kupokea rushwa ili sheria iweze kufuata mkondo wake wa kuwakamata wahusika ambao wamekuwa na tabia kama hiyo.
AdTech Ad

0 maoni:

Chapisha Maoni