Ijumaa, 15 Aprili 2016

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI KUWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA BARABARA YA JUU (FLYOVER) YA TAZARA NA KUFUNGUA DARAJA LA KIGAMBONI JIJINI DARA ES SALAAM


taza
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya TAZARA na ufunguzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Siku ya Jumamosi tarehe 16 Aprili, 2016 Mheshimiwa Rais ataweka jiwe na msingi la ujenzi wa barabara ya juu katika makutano ya barabara Nyerere na Mandela (Flyover ya TAZARA).
Jumanne tarehe 19 Aprili, 2016 Mheshimiwa Rais atafungua rasmi Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5.  Ujenzi huu umefanywa na Kampuni ya China Railway 15 Group ilishirikiana na Kampuni ya China Bridge Engineering Group.
Aidha wakati tunasubiri uzinduzi rasmi, Wananchi na magari yenye uzito usiozidi tani 10 yataruhusiwa kutumia Daraja la Kigamboni kuanzia Jumamosi tarehe 16 Aprili, 2016 ili kuwawezesha kuelewa vizuri miundombinu na matumizi ya daraja.
Utekelezaji wa miradi hii ni mojawapo ya jitihada za Serikali za kuboresha miundomninu na kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam.
Imetolewa na;
Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu  (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
14 Aprili, 2016
AdTech Ad

0 maoni:

Chapisha Maoni