Ijumaa, 15 Aprili 2016

MWAKILISHI MPYA WA UNHCR NCHINI AJITAMBULISHA KWA WAZIRI KITWANGA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

W1Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati), akimkaribisha ofisini kwake Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya wakati alipokuwa anawasili ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha kwa Waziri huyo mara baada ya kuteuliwa na Shirika lake kuja kuiongoza UNHCR nchini. Hata hivyo, viongozi hao katika mazungumzo yao walijadiliana masuala mbalimbali jinsi wa kuwahudumia wakimbizi waliopo nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke.
W2Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia), akimfafanulia jambo Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya wakati Mwakilishi huyo alipomtembelea Waziri Kitwanga ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha baada ya kuteuliwa na UNHCR kuja kuwa kiongozi wa Shirika hilo nchini.
W3Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akimfafanulia jambo Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (kulia) wakati Mwakilishi huyo alipomtembelea Naibu Waziri huyo ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha baada ya kuteuliwa na UNHCR kuja kuwa kiongozi wa Shirika hilo nchini. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke. Katikati ni Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika hilo, Yoko Akasaka, na Afisa wa Shirika hilo nchini, Daria Santoni (wa pili kulia).
W4Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (kushoto) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga wakati Mwakilishi huyo mpya nchini alipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha mara baada ya kuteuliwa na UNHCR kuwa kiongozi wa Shirika hilo nchini.
W5Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (katikati), pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke. Kapaya ameteuliwa na UNHCR kuwa Mwakilishi wa Shirika hilo nchini na amemtembelea Waziri Kitwanga ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha, hata hivyo katika mazungumzo yao walijadiliana masuala mbalimbali ya jinsi ya kuwahudumia Wakimbizi waliopo nchini.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

0 maoni:

Chapisha Maoni