Mbunge wa
Jimbo la Mufindi kusini Mhe, Mendrad Kigola ameanza kuchukua hatua za kupambana
na tatizo la vifo vya Wajawazito na Watoto wachanga kwa kuboresha baadhi ya
vitio vya afya katika jimbo lake.
Kigola
aliyasema hayo jana wakati akizungumza na mwandishi wa mtandao huu wa Kali ya habari kuhusu
utekelezaji wa majukumu yake kutokana na vifo vya wajawazito na watoto wachanga
vinavyotokana na uzazi.
‘’Mimi
nimeshaanza hatua zakupambana na tatizo hili na tayari nimeboresha vituo
saba vya afya katika jimbo langu kikiwemo kituo cha afya nyololo na Malangali
.
“Lakini
kuboresha zahanati na vituo vya afya pekee haitoshi ila inatakiwa kuboresha
miundombinu, umeme na maji huko vijijini ndipo afya inakuwa imekamilika.
Nitaishawishi serikali ihakikishe fedha inatolewa kwa ajili ya maendeleo hayo”
alisema Kigola
Alisema katika Bunge lijalo la
bajeti atahakikisha anasimamia Wizara ya afya ili kuhakikisha fedha inayo
tengwa inaelekezwa kwenye ujenzi wa zahanati na vituo vya afya kama njia moja
wapo ya kutatua tatizo hilo katika jimbo lake na Tanzania nzima kwa ujumla
Mhe, Kigola
alisema katika mikakati yake ataishauri Serikali kuboresha Zahanati na vituo
vya afya ili ifikapo mwaka 2025 tatizo la vifo vinavyotokana na uzazi liwe
limepungua kama si kuisha kabisa
“Suala kubwa
ni kuihamasisha serikali kuboresha vituo vya afya na zahanati kwa kuhakikisha
kunakuwa na wataalam na dawa katika vituo hivyo ili akina mama wasipate shida
pale unapofika wakati wao wa kujifungua” alisema
Hata hivyo
alisema kuboresha zahanati na vituo vya afya pekee haitoshi atahakikisha
pia Serikali inaboresha miundombinu na kupeleka umeme na maji huko vijijini ili
kurahisisha kazi ya utoaji wa huduma ya afya
Aidha alisema serikali inapaswa
kuliona tatizo hili kama ni suala la muhimu na kuchukua hatua kwani ukitokea
uzembe na kuchukuliwa mzaha tatizo linaweza kuwa kubwa zaidi na likasababisha
hasara kubwa kwa Taifa.
Alisema watu wanapoongezeka bajeti
pia huongezeka na kwamba serikali inatakiwa kuwa na bajeti ya kutosha ili
kukidhi ongezeko la watu linalojitokeza
Hii ni kutokaa na kuonesha kuwa
Tanzania ina watu milioni 45, watu milioni moja huongezeka kila mwaka ambapo
inakadiliwa ongezeko la watu litakuwa mara tatu zaidi kila mwaka na kufikia
watu milioni 130 ifikapo mwaka 2050
Hata hivyo alisema wananchi
wanatakiwa kupanga uzazi katika uwiano mzuri ili kuwa na watoto wenye afya
kuliko kubananisha watoto wasio kuwa na afya hali ambayo humuathiri hata mzazi.
“Tunapozungumzia
uzazi wa mpango, ni suala pana kwa sababu kila mtu ana hoja yake lakini cha
msingi ni kwamba, tunaposema watu watumie uzazi wa mpango tunamaanisha kuwa
watu wazae watoto wenye interval (uwiano) mzuri kwa sababu kuna watu kila mwaka
anataka kuwa na mtoto sasa hiyo haifai, Tunataka watoto wapishane vizuri kiafya
wasibanane mno” alisema
0 maoni:
Chapisha Maoni