Mbunge
wa Kilombero Peter Lijuakali afanya mkutano na wafanyakazi wastaafu wa
Illovo wa Kilimo cha miwa mapema jana Aprili 17.2016.
Katika
mkutano huo, Mbunge huyo Peter Lijuakali aliweza kukutana na Wazee wa
Kidatu na kujadiliana nao namna ya kumaliza mgogoro wa Wafanyakazi
wastaafu wa kiwanda cha Miwa cha Illovo pamoja na suala zima la kilimo
cha miwa.
Pia aliweza kujadiliana nao mambo ya Afya, kilimo kwa ujumla na mambo mengine mengi ya kimaendeleo katika jimbo hilo.
“Changamoto
za jimbo ni nyingi sana kiasi kwamba ninashawishika kuamini kuwa
Kilombero ni kama haikua na Mbunge kabisa. Hatua kwa hatua tutazikabili
changamoto hizi” alieleza Peter Lijuakali katika taarifa yake wakati
alipokutana na wananchi wa jimbo lake hilo.
Peter
Lijuakali amekuwa mstari wa mbele katika kufanikisha kuleta maendeleo
ndani ya jimbo lake hilo tokea achaguliwe kwani amekuwa akisaidiana na
wananchi katika shida na mambo mbalimbali ya kijamii.






0 maoni:
Chapisha Maoni