Jumanne, 19 Aprili 2016

Jide ampeleka Ray C kwenye maombi


jide na ray c1
Jide (kushoto) akiwa na Ray c (katikati) pamoja na shoga yao.
STORI:  Musa Mateja na Sifael Paul, Wikienda
Dar es Salaam: Tenda miujiza Bwana! Lile sakata la mwanadada Rehema Charamila ‘Ray C’ kuandamwa na pepo mbaya wa utumiaji wa dawa za kulevya ‘unga’ hata baada ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ‘JK’ kumsaidia, inasemekana Mwanamuziki Judith Wambura ‘Jide’ ameambatana naye kanisani kwa ajili ya maombi.

Kikimwaga ‘ubuyu’ mbele ya Ijumaa Wikienda, chanzo chetu kilitonya kuwa hivi karibuni Ray C alitinga nyumbani kwa Jide, Masaki jijini Dar kwa ajili ya kumsalimia na kumpa hongera kwa wimbo wake mpya wa Ndi Ndi Ndi, lakini wakati huohuo kukawa na dada anayefahamika kwa jina la Anitha ambaye huwa anasali na Ray C.
lady jay dee na ray c….Wakiwa kwenye pozi.
Ilifahamika kwamba Anitha ni rafiki wa Ray C na pia wa Jide hivyo ulipofika muda wa kwenda kwenye maombi ndipo Jide akaungana na Anitha kumpeleka Ray C kanisani kwa ajili ya maombi.
“Jide na Ray C wana muda mrefu sana hawajaonana kwa zaidi ya miaka mitano au sita ila hivi karibuni Ray C alikuja nyumbani kwa Jide (Masaki) kwa ajili ya kumsalimia na kumpa pongezi kwa wimbo wake mpya ndipo Jide alipojumuika kumpeleka Ray C kanisani kwenye maombi ingawa nasikia kuna watu wengi ambao wanamsaidia Ray C na muda mwingi anaenda kanisani kwa ajili ya maombi,” kilisema chanzo hicho.
Kwa upande wake, meneja wa Jide, Christina Mosha ‘Seven’ alithibitisha Jide kutembelewa na Ray C kisha kwenda kanisani kwa maombi.

0 maoni:

Chapisha Maoni