Droo
ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup),
inatarajiwa kufanyika kesho Jumanne saa 3 usiku moja kwa moja (live)
kupitia kituo cha luninga cha AzamTwo.
Hatua
ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) itafanyika live katika
kituo cha AzamTwo, ambao kupitia Azamtv ndio wadhamini wa wakuu wa
michuano hiyo iliyoibua msisimiko wa mpira wa miguu na kushirikisha timu
nyingi zaidi nchini.
Baada
ya timu za Azam FC, Mwadui FC, na Yanga SC kukata tiketi ya kucheza
Nusu Fainali, mshindi wa mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Coastal Union
utakaochezwa leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam atungana na
timu hizo tatu kwenye droo ya leo






0 maoni:
Chapisha Maoni