Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Ijumaa, 30 Septemba 2016

Rais Magufuli afunga Maadhimisho ya Miaka 52 ya JWTZ ashuhudia Zoezi la Amphibious Landing Bagamoyo

Posted by Esta Malibiche on Oct.1 2016 in NEWS
j1
Amiri  Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akipiga ngoma za bendi ya jeshi ya Mwenge Jazzz wana Paselepa wakati  wa kufunga Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
j2
 Amiri  Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na meza kuu wakipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa wakati wa kufunga Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
j3
 Ndege vita zikipita angani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
j4
 Ndege vita zikipita angani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
j5
Amiri  Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na meza kuu wakipiga makofi wakati wa Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016.PICHA NA IKULU.
…………………………………………………………………………………
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Septemba, 2016 amefunga maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kushuhudia zoezi la medani liitwalo ”Amphibious Landing” lililofanyika katika Kijiji cha Baatini Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Zoezi hilo lililochukua muda wa wiki mbili, limeshirikisha kamandi zote tano za JWTZ  ambazo ni Nyika, Majini, Anga, Kamandi ya Makao Makuu na  Jeshi la Kujenga taifa limefanyika katika ufukwe wa bahari ya Hindi na limetekelezwa kwa mfano wa mapambano ya kivita yaliyohusisha kutua nchi kavu kutoka majini na kukomboa eneo lililotekwa.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Rais na Amiri jeshi Mkuu Dkt.John Pombe Magufuli amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange pamoja na Makamanda na Wapiganaji wote wa JWTZ walioshiriki katika zoezi hilo ambalo limefanywa kwa umakini, uhakika na weledi wa hali ya juu.
”Kwa kweli nimefurahi na nimeamini tuna wapiganaji wa kutosha katika maeneo yote, hii
mikakati na mipango iliyotumika inaonesha tuna jeshi imara na linaloaminika” amesema Dkt. Magufuli. 

Rais na Amiri Jeshi Mkuu amewahakikishia Makamanda na Wapiganaji wote wa JWTZ kuwa Serikali yake itahakikisha inaendeleza na kuongeza zaidi juhudi zilizofanywa na Marais waliopita kwa kuimarisha na kuwa na jeshi la kisasa linalotumia vifaa na teknoljia ya kisasa na pia itahakikisha maslai ya askari yanaboreshwa.
Aidha, Dkt. Magufuli ametaka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuimarishwa zaidi na kujielekeza
katika uzalishaji mali ikiwemo uwekezaji katika viwanda.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ambaye pamoja na kuipongeza  JWTZ amesema miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi hilo Watanzania wanashuhudia jeshi lao likiwa imara na makini zaidi kwa ajili ya kulinda nchi.
Nae Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange amemshukuru Rais na Amiri Jeshi
Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake na nia yake ya kuliimarisha Jeshi na kuboresha maslai ya Makamanda na Wapiganaji na ameongeza kuwa anajivunia kuwa kiongozi  wa Jeshi hilo.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Viongozi wengine wakiwemo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Abdulhamid Yahaya Mzee.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, amemuagiza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kuwapa ajira za JWTZ askari mgambo wote walioshiriki zoezi la Amphibious Landing, Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Dar es Salaam

WAZIRI MKUU ATIMIZA AHADI YA KUHAMIA DODOMA

Posted by Esta Malibiche Oct 1.2016 in SIASA

don
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwapungia akiwapungia wananchi wa Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea ufunguo ikiwa ni ishara ya kukaribishwa Dodoma na Meya wa Manispaa ya Dodoma Jafar Mwanyemba katika mapokezi yaliyofanyika kwenye makazi yake , Mlimwa Septemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha ufunguo aliokabidhiwa na Meya wa Manispaa ya Dodoma, Jafar Mwanyemba (kushoto) kuashiria kupokewa rasmi kwenye manispaa hiyo. Makbidhiano hayo yalifanyika kwenye makazi yake eneo la Mlimwa Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa Dodoma baada ya kukaribishwa kimira na wazee hao Septemba 30, 2016.
Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akizawadiwa kimira na wanawake wa Dodoma ikiwa ni ishara ya kumkaribisha karika Manispaa hiyo, Septemba 30, 2016.
Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akizawadiwa kimira na wanawake wa Dodoma ikiwa ni ishara ya kumkaribisha karika Manispaa hiyo, Septemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa na mkewe Mary wakiagana na watuimishi wa Makazi ya Waziri Mkuu ya Dar es salaam kabla ya kuondoka kuelekea Dodoma Septemba 30, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisalimiana na Madiwani wa Manispaa ya Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisalimiana na Madiwani wa Manispaa ya Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kasim Majliwa akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye makazi yake mjini Dodoma Septemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi wa Dodoma wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye makazi yake eneo la Mlimwa Septemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………………
Waziri MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzia sasa mtu yeyote mwenye shida ya kuonana naye itabidi amfuate Dodoma na kwamba atarudi Dar es Salaam pindi akiitwa na Mheshimiwa Rais au Makamu wa Rais.
Ametoa kauli hiyo leo jioni (Ijumaa, Septemba 30, 2016) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali na wakazi wa mji wa Dodoma waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili mjini hapa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa Julai 25 kuwa atahamia Dodoma ifikapo Septemba mwaka huu.
“Tukio hili la kuhamia Dodoma si la mzaha, hakuna siasa na wala si jaribio. Tumeshakeleza. Kama kuna waliokuwa wanafiria kwamba halitekelezeki watambua kwamba tayari tumeshafika. Na kuanzia sasa atakayetaka huduma ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu amesema Dodoma si ndogo kama baadhi ya watu wanavyodai na kwamba  huduma zilizopo zinatosha kukidhi mahitaji ya sasa. “Mkakati uliopo wa kupanua huduma za tiba, maji, umeme na masoko utawezesha watumishi wote kuishi bila bugudha yoyote.”
“Awamu ya kwanza inaanzia Septemba hadi Februari mwakani. Mimi nimeshatangulia na wanaofuata ni mawaziri na manaibu wao wote, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wote. Natambua kwamba wote wana nyumba za kuishi na kama wapo ambao hawana hawazidi asilimia tano na nyumba zipo
Amewataka watumishi wote wa Serikali watambue kwamba safari imeshaanza na kila mmoja ajipange, na akarudia wito wa Mheshimiwa Rais kwamba atakayegoma kuhamia Dodoma atakuwa amejifukuza kazi.
Waziri Mkuu amewataka watendaji wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) wasifanye kazi kwa mazoea, bali wabadilike na kwa kuwa amehamia Dodoma ameahidi kuafuatilia kwa karibu zaidi.
Mapema akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Nchi (OWM SUBKAV), Jenista Mhagama amesema kilichofanyika leo ni uthibitisho kuwa yale ambayo Serikali ya Awamu ya Tano iliahidi sasa hivi imeanza kuyatekeleza.
“Tuliahidi kukusanya kodi, tuliahidi elimu bure, tuliahidi kupambana na mafisadi, tuliahidi kuondoa watumishi hewa, tuliahidi kuifufua ATCL na kununua ndege mpya na yote tumetekeleza,” amesema.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. George Simbachawene amesema uamuzi wa kuhamia Dodoma ni uthibitisho kuwa  viongozi wetu kweli wamedhamiria kutekeleza ahadi ya Baba wa Taifa ya kuhamishia makao makuu ya nchi hapa Dodoma.
“Dodoma imeanza kuchangamka na hii ni fursa tosha kwa mkoa wetu kubadilika. Tushirikiane na CDA kuijenga Dodoma mpya. Kitendo cha Mheshimiwa Waziri Mkuu kuingia Dodoma leo hii maana yake ni kwamba Serikali iko rasmi Dodoma,” amesema.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Manaibu Waziri Anthony Mavunde na Dk. Ashatu Kijaji, Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais (Utumishi), Wakuu wa Wilaya za Mkoa huo, wazee wa mkoa huo, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi zilizoko mkoani na baadhi ya wananchi.

SOMA MAGAZETI YA LEO HAPA.Oct 1

Posted by Esta Malibiche on Oct 1,2016 in





UK

LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA WIKIENDI HII

Posted by Esta Malibiche on Sept30.2016 in MICHEZO

2
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inaendelea leo Septemba 30, 2016 kwa mchezo mmoja tu, unaozikutanisha timu za Toto Africans na Ndanda ya Mtwara katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kama ilivyo kwa leo, kesho pia kutakuwa na mchezo mmoja tu utakaowakutanisha watani wa jadi, Young Africans na Simba katika dimba la Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo, umekuwa na hamasa ya aina yake.
Lakini kwa siku ya Jumapili, michezo itakuwa mitano ambako Mbe
ya City itaikaribisha Mwadui kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya; Majimaji itakuwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati African Lyon itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Mvomero mkoani Morogoro.
Mbao baada ya kucheza na Ruvu Shooting wiki iliyopita, ilibakia Mlandizi mkoani Pwani kusubiri kucheza na JKT Ruvu Jumapili kwenye Uwanja wa Mabatini huko Mlandizi wakati Kagera itaikaribisha Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.

NAIBU WAZIRI MPINA AMUUNGA MKONO MAKONDA KATIKA ZOEZI LA KUPANDA MITI.

Posted by Esta Malibiche on Sept30.2016 in NEWS

luh1
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akipanda mti katika shule ya Sekondari ya Mama Salima Kikwete iliyopo Kijitonyama Jijini Dar es salaam ikiwa ni ishara ya kuunga mkono kampeni ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ya kupanda miti                       
luh2
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiongea na wanafunzi mara baada ya kumaliza zoezi la kupanda miti katika shule ya sekondari ya Mama Salima Kikwete.                          
luh3
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh Luhaga Mpina akifafanua jambo mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mama Salima Kikwete.
……………………………………………………………..
EVELYN MKOKOI
 Kuelekea siku ya uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti jijini  Dar es salaam maarufu kama “mti wangu’, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Ameunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda katika Jitahada zake za kutunza mazingira kwa kupanda miti.
Naibu Mpina ameshiriki kwa kutangulia kupanda mti leo katika shule ya sekondani ya Salma Kikwete iliyopo kijitonyama jijini Dar es Saalam, ambapo wakala wa misitu nchini wametoa miti 600 ili kukamilisha zoezi hilo katika shule hiyo ya sekondari.
Naibu Waziri amewataka wakuu wote  wa mikoa na wilaya kuiga jitihada za Mhe. Makonda na  kuacha tabia za mazoea zilizojitokeza huko nyuma za kutoa taarifa za uwongo katika Ofisi ya Makamu wa Rais Kuwa Miti kadhaa imepandwa lakini ki uhailisia hakuna kilichofanyika.
Aidha ametoa wito kwa watendaji wa serikali wanaochakachua maaagizo ya viongozi na kusema kuwa serikali hii ipo makini hivyo kutakuwa na ufuatiliaji kwa  kila Mkoa, Wilaya na Halmashauri kwani zoezi hili la upandaji miti ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama tawala.
“Hatutavumilia kuona miti inakatwa ovyo, misitu inachomwa moto na viongozi wa serikali wakilifumbia macho suala hilo.” Alisisitiza.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugezi wa Wakala wa Misitu Nchini  Profesa Santos Silayo alisema, Taasisi hiyo imetoa jumla ya miche ya miti 8000 ili kukamilisha zoezi hilo katika jiji la Dar es Salaam, na kumpongeza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kuonyesha mwanzo mpya na jitihada katika jiji la Dar es Salaam kwa kupanda miti na kutunza mazingira.
Bi Jacquline Wolper Muhamasishaji wa swala la utunzaji wa mazingira na muigizaji maarufu nchini, akishiriki zoezi hilo, kwa kupanda miti amepongeza jitihada za mkuu wa Mkoa Makonda kwa kuzunguka katika mashule mbalimbali jijini kuhamasisha zoezi hilo kwa kutoa miche ya miti

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI KUFANYIKA TAREHE 1/10/2016

Posted by Esta Malibiche on Sept30.2016


index
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, inatoa taarifa kuwa, tarehe 1 Oktoba ya kila mwaka, ni kilele cha  Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani. Katika siku hii, Tanzania inaungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku hii kwa mujibu wa Azimio la Umoja wa Mataifa Na. 49 la mwaka 1991. 
Maadhimisho ya siku ya wazee duniani ni moja kati ya jitihada za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) katika kutambua na  kuhamasisha jamii kuweza kulinda na kutetea haki za wazee duniani kote.  Umoja wa Mataifa umetenga siku hii kwa lengo la kutafakari hali ya maisha ya wazee na changamoto zinazowakabili wazee; na hivyo kuweka mipango thabiti ya kuboresha maisha yao na kuwafanya waishi maisha ya heshima, hadhi, na kuthaminiwa utu wao. 
Kila mwaka, Maadhimisho haya huwa yanabeba Kauli Mbiu yenye ujumbe mahsusi. Kwa mwaka 2016 Kaulimbiu inasema “Zuia Unyanyasaji dhidi ya Wazee”. Kaulimbiu hii inahimiza Serikali, jamii, na wadau wengine kutafakari na kuweka mikakati ya kukabiliana na vitendo vya ukatili, mauaji, ubaguzi na dhuluma dhidi ya wazee; vitendo ambayo ni kinyume dhidi ya haki za binadamu.
Maadhimisho haya kwa mwaka 2016 yanafanyika Kitaifa katika wilaya ya Mbalali, mkoani Mbeya. Kilele cha maadhimisho haya kitajumuisha shughuli mbalimbali ikiwemo huduma ya upimaji wa hiari wa afya na ushauri kwa wazee, michezo na maonesho ya bidhaa na kazi mbalimbali zinazofanywa na wazee.
Katika kipindi hiki cha Maadhimisho hatuna budi kuenzi na kudumisha mila na desturi nzuri za kuwaenzi wazee kwa kutambua kuwa wazee ndiyo chanzo cha urithi wa historia ya nchi, washauri wa familia na jamii, watu wenye hekima, na walezi katika jamii. Hivyo jamii inaowajibu wa kuwaondolea vikwazo wazee katika kupata huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua pale ambapo mzee ananyanyashwa au kutendewa isivyostahili.
Erasto T. Ching’oro
Msemaji wa Wizara
30/9/2016

WAREMBO 30 MISS TANZANIA WATINGA KAMBINI LEO, WAPEWA SOMO LA AWALI NA MISS TANZANIA WA SASA

ware
Baadhi ya Washiriki watakaowania Taji la Miss Tanzania 2016 wakiwa katika picha pamoja muda mfupi baada ya kuwasili kambini. Jumla ya Washiriki 30 kutoka kanda mbalimbali nchini wameingia Kambini leo Septemba 30, 2016 tayari kwa maandalizi ya Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi ujao.
Mrembo anaeshikilia Taji la Miss Tanzania kwa sasa, Lilian Kamazima akizungumza na Warembo alipokutana nao leo Septemba 30, 2016 kwenye Hoteli ya Regency, Jijini Dar es salaam. ambapo jumla ya Washiriki 30 wameingia kambini leo tayari kwa maandalizi ya Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi ujao.
Baadhi ya Washiriki wa Miss Tanzania 2016 wakimsikiliza kwa makini Mrembo anaeshikilia Taji la Miss Tanzania kwa sasa, Lilian Kamazim.
 Warembo wakifanyiwa Usaili na viongozi wa Miss Tanzania.

WIZARA YA AFYA YAUPONGEZA MKOA WA SINGIDA KWA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA KATIKA NGAZI YA HALMASHAURI

Posted by Esta Malibiche on Sept30.2016 in NEWS

msin
Grace Singida.
Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee imeishauri mikoa yote ya Tanzania bara kuiga mfano wa mkoa wa Singida wa kuanzisha huduma za kibingwa za mkoba kwa ngazi za wilaya ili kuwafikia watanzania wengi wenye uhitaji.
Mkurugenzi wa tiba kutoka wizara hiyo Dokta Magreth Mhando ametoa ushauri huo katika hospitali ya Mtakatifu Calorus Mtinko Singida Vijijini alipotembelea kujionea awamu ya pili ya zoezi la huduma za kibingwa za Mkoba.
Dokta Mhando amesema kumekuwa na huduma za kibingwa za mkoba ila hazikufanyika  vizuri kama ambavyo mkoa wa Singida umekuwa ukifanya na kutoa pongezi za Wizara kwa Mkuu wa mkoa na Mganga mkuu wa mkoa kwa ubunifu huo.
Amesema huduma za kibingwa za mkoba zimekuwa zikiratibiwa na taasisi au hospital kubwa kama Muhimbili ambapo madaktari bingwa wamekuwa wakitoa huduma kwa ugonjwa fulani na kwa ngazi ya hospitali za Mkoa tofauti na zoezi linaloendelea Mkoani Singida la kutoa huduma za kibingwa kwa magonjwa mbalimbali.
Dokta Mhando ameongeza kuwa kutokana na uhaba wa madaktari bingwa nchini wizara imetenga fedha kwa ajili ya kuwasomesha madaktari na kuwashauri waajiri ambao ni makatibu tawala wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya kuwasomesha madaktari hao kwakwuwa wizara pekee haitaweza.
Amesema utaratibu ni kuwa na madaktri bingwa angalau watano kila Mkoa lakini mikoa mingi haina idadi hiyo huku akiongeza kuwa lengo la kutembelea zoezi hilo Singida nikujionea hali halisi na sio kusubiria taarifa.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe mara baada ya kutembelea wodi zote na kuzungumza na wagonjwa waliopata huduma za kibingwa amemtaka Mganga Mkuu wa Mkoa kuongeza muda wa kutoa huduma hiyo kutoka siku tano hadi nane kutokana na wingi wa wagonjwa waliojitokeza.
Mhandisi Mtigumwe amesema huduma hiyo inasaidia kutambua magonjwa na kuyatibu kabla hayajawa sugu lakini pia gharama zikiwa nafuu kutokana na kusogezwa kwa ngazi za halmashauri.
Ameongeza kuwa lengo la ofisi yake ni kuhakikisha huduma za kibingwa za mkoba zinapelekwa kwa kila halmashauri na endapo zoezi likikamilika na kukiwa na uhitaji mkubwa kuna uwezekano mkubwa wa kurudia zoezi hilo.
Mhandisi Mtigumwe amesema kuelekea Tanzania ya viwanda afya bora ni muhimu na wazalishaji wakubwa ni wananchi wa ngazi za chini hivyo huduma hiyo itasaidia kuimarisha afya ili waweze kuzalisha  bidhaa kwa wingi na zenye ubora.
Amesema kwa wale wagonjwa watakaopewa rufaa kwenda nje ya Mkoa utaratibu utaangalia wa kuwapatia usafiri wa Mkoa ili kuwapeleka hasa wale wasiojiweza.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta John Mwombeki amesema kwa muda wa siku tano wagonjwa zaidi ya 800 wameonana na madaktari bingwa huku idadi ikitarajiwa kuongezeka kutokana nakuongezwa kwa siku za klutoa huduma.
Dokta Mwombeki amesema wagonjwa wengi wanaofika wanatoka maeneo mbalimbali hasa maeneo ya kijijini na wenye hali duni ya maisha hivyo zoezi hilo limesaidia wananchi hasa wwenye kipato cha chini.
Amesema madaktari bingwa wanaotoa huduma za kibingwa za mkoba ni madaktari bingwa wa magonjwa ya akina mama, watoto, macho, meno, magonjwa ya ndani na daktari bingwa wa upasuaji.
Wagonjwa waliopata huduma wameushukuru uongozi wa mkoa kwa kubuni utaratibu wa kuwafuata wagonjwa karibu ili kuwapatia huduma za kibingwa kwakuwa inawasaidia kupata matibabu mapema kabla magonjwa hayajawa sugu na kushauri huduma iwe endelevu angalau kila mwaka.