Muonekano
wa kivuko cha MV. Malagarasi kilichopo katika eneo la Ilagala mkoani
Kigoma. Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 100, magari sita na
tani 50 kwa wakati mmoja.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu
kushoto), akipata maelezo ya kivuko cha MV. Malagarasi kutoka kwa
Msimamizi wa Kivuko hicho kabla ya kukikagua. Kulia ni Meneja wa Wakala
wa Barabara nchini (TANROADS), mkoani kigoma Eng. Narcis Choma na Wa
pili kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akishuka
katika Kivuko cha MV. Malagarasi mara baada ya kukikagua na kuona namna
ya kivuko hicho kinavyofanya kazi.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili
kulia), akioneshwa vifaa vya uokoaji katika kivuko cha MV. Malagarasi.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto)
akijadiliana jambo na mmoja wa abiria wa Kivuko cha MV. Malagarasi.
Meneja
wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS, mkoani kigoma Eng. Narcis Choma
(wa tatu kushoto) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), barabara ya Simbo-Kalya yenye
urefu wa zaidi ya Km 200 Kusini mwa Ziwa Tanganyika itakayoanza kujengwa
hivi karibuni wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa wananchi wa Ilagala, Sunuka, Karago, Herembe,
Kapalamsenga, Mgambazi, Lukoma hadi Kashagulu ya namna sahihi ya kutumia
kivuko cha MV. Malagarasi, mkoani Kigoma.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza
kulia), akioneshwa namna ya huduma za uongozaji ndege zianvyofanyika
katika kituo cha Kigoma. Kushoto ni Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga
mkoani Kigoma Bw. Godlove Longole na katikati ni Mbunge wa Kigoma Mjini
Mhe. Zitto Kabwe akifatilia.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia),
akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga mkoani
Kigoma Bw. Godlove Longole wakati alipokagua Uwanja wa Ndege mkoani
hapo. Wa pili kulia ni Mbunge wa kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe
akifatilia.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto),
akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Nchini (TRL)
Bw. Masanja Kadogosa (kulia), wakati wa mkutano na wafanyabiashara
wanaosafirisha bidhaa zao katika mwambao wa Ziwa Tanganyika, mkoani
Kigoma.
Wafanyakazi
wa Kampuni ya Simu nchini (TTCL) katika picha ya pamoja na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati
waliokaa). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
0 maoni:
Chapisha Maoni