Jumatano, 5 Oktoba 2016

ZAHANATI YA MIHUGA YAPATA GARI LA KUBEBEA WAGONJWA




Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, akiwasha gari kama ishara ya kuonyesha umadhubuti wa gari lililotolewa na Bwana Abdallah Saad kwa ajili ya Zahanati  ya kijiji cha Mihuga.
Mjumbe wa kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Bagamoyo, Ndg. Mkang’ata akitoa neno la shukrani kwa niaba ya chama cha Mapinduzi
Bwana Abdallah Saad  (aliyesimama) aliyetoa Gari hilo akizungumza baada ya kutoa gari na  jinsi alivyopokelewa  kijiji hapo na mashirikiano mazuri waliyonayo na wanakijiji na kwa nini amechangia gari hilo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani kikwete akiwa na Daktari wa Zahanati ya kijiji cha Mihuga wa kwanza kushoto wa tatu kutoka kushoto ni  Diwani wa kata ya Miono Ndg. Juma Mpwimbwi na wa kwanza Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Alhaj Majid Mwanga
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani wa pili kutoka kushoto akiwa na baadhi ya viongozi walioshiriki makabidhiano ya gari la wagonjwa katika zahanati ya Kijiji cha Mihuga.
Mbunge Kikwete akionyesha funguo baada ya makabidhiano na akiwa mwekezaji Bwana Abdallah Saad aliyetoa gari hilo.
Mbunge Ridhiwani Kikwete aliyesimama akitoa shukrani zake kwa  Bwana Abdallah Saad aliyetoa gari hilo.

0 maoni:

Chapisha Maoni