Posted by Esta Malibiche on Oct4.2016 in SIASA
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah
Ulega akikagua jengo linalotarajiwa kuwa shule mpya katika kitogoji cha
kikonga katika ziara yake kijiji kwa kijiji kwa kushukuu wananchi kwa
kumchagua pamoja kuangalia maendeleo leo katika Kijiji cha Bupu Wilaya
ya Mkuranga mkoani Pwani.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah
Ulega akizungumza na wananchi katika kitongoji cha Kikonga akiwa ziara
yake kijiji kwa kijiji kwa kushukuu wananchi kwa kumchagua pamoja na
kuangalia maendeleo leo katika Kijiji cha Bupu Wilaya ya Mkuranga.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah
Ulega akizungumza katika mkutano wa wananchi wa kitogoji cha Kikonga juu
ya changamoto zinazowakabili akiwa ziara yake kijiji kwa kijiji kwa
kushukuu wananchi kwa kumchagua pamoja kuangalia maendeleo leo katika
Kijiji cha Bupu Wilaya ya Mkuranga.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah
Ulega akiwaonyesha wananchi Diwani wao,Abbas Msangule jinsi ya
kushirikiana naye kwa maendeleo katika Kijiji cha Kondo Mwelazi katika
ziara yake kijiji kwa kijiji kwa kushukuu wananchi kwa kumchagua pamoja
kuangalia maendeleo leo katika Kijiji cha Bupu Wilaya ya Mkuranga mkoani
Pwani.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah
Ulega akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya msingi Kondo
Mwelazi alipowatembelea kujua mazingira walionayo na kuwashukuru
kuendelea na moyo licha ya kuwa na mazingira mgumu leo.
…………………………………………………………..
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amewataka wananchi kufanya maendeleo na sio siasa kwa muda huu.
Hayo ameyasema leo katika
katika ziara ya vijiji vya kata ya bupu, Ulega amesema kuwa wakati
umefika kwa kabila yake kusomesha watoto kwa ajili ya maendeleo kutokana
dunia ya sasa inahitaji watalaam.
Ulega amesema kuwa changamoto
zilizo katika kata ya Bupu ni maji pamoja na miundombinu ya barabara
hivyo vinatakiwa kupatiwa ufumbuzi ili wananchi waondokane na changamoto
hizo.
Mbunge huyo ameahidi kutoa
Bati 50 katika shule mpya inayojengwa katika kitongoji cha kikonga
kutokana watoto wa kitongoji hicho wanatembea kilomita sita.
Ulega amesema changamoto zilizopo wilaya ya mkuranga zinatakiwa zitatuliwe kutokana na kuomba kazi ya kuwatumikia wananchi.
Amesema kuwa suala mfuko wa afya ya jamii CHF dawa hazipatikani na kufanya wananchi wengine washindwe kujiunga.
Aidha amesema wananchi
waliojiunga na CHF ni 65 ikiwa nia serikali ni watu wote wajiunge ili
wasipate adha ya kupata huduma za afya.
Hata hivyo amesema nia ya
Rais Dk. John Pombe Magufuli ni kuona wananchi wanafurahia huduma
zinazotolewa na serikali na sio vinginevyo.
waakuu mdawenu
0 maoni:
Chapisha Maoni