Posted by Esta Malibiche on Oct4.2016 in NEWS
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika
Wilaya Iramba Mkoani Singida na kukagua huduma za Afya katika Hospitali ya
Wilaya pamoja na Zahanati ya Kisimba ndani ya Wilaya hiyo.
Katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla ameweza kubaini
mapungufu mbalimbali ambayo ameagiza yapatiwe ufumbuzi ndani ya miezi mitatu.
Akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba, ameweza
kujionea huduma mbalimbali zitolewazo Hospitalini hapo hata hivyo ameagiza
uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanafunga mfumo wa ukusanyaji mapato wa
malipo wa kisasa kwa njia ya kielektroniki.
“Mfumo wa malipo ya kielektroniki umeleta ukombozi
mkubwa sana kwenye mahospitali nchini. Mapato yameongezeka. Udhibiti wa mapato
umekuwa rahisi. Nawaagiza nanyi Hospitali ya Iramba kuhakikisha munafunga mfumo
huu wa malipo wa kisasa hususani kwenye: Maabara,Chumba cha upasuaji (Theatre),
Dirisha la dawa, na sehemu zote zenye kuingiza mapato”. Ameeleza Dk.Kigwangalla
wakati wa kutoa maagizo hayo.
Katika Zahanati ya Kisimba ambayo ipo umbali wa
zaidi ya Kilometa 10, Dk.Kigwangalla ameweza kujionea huduma mbalimbali kwenye
Zahanati hiyo ambayo ni mpya huku ikiwa msaada mkubwa kwa wananchi wa vijiji
hivyo.
mwisho
.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akisiliza maelekezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa
Hospitali ya Iramba, Mkoani Singida wakati alipotembelea chumba cha
upasuaji Hospitali hapo.
Picha chini ni Majengo ya Zahanati mpya ya Kisimba iliyopo Wilayani Iramba.






0 maoni:
Chapisha Maoni