Kampuni ya EM & U Investment imeandaa tamasha la Chakula na Vinywaji litakalofanyika (Dar es Salaam Food & Drink Festival) Jumamosi hii ya Oktoba 8, 2016  katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Edward James amesema tamasha hilo litakuwa la aina yake kwa kushirikisha wapikaji  wa vyakula vya asili ikiwa ni kufanya Watanzania kuvipenda vyakula hivyo.
Na kuongeza kuwa watu wengi wanapenda kula vyakula vya asili lakini hawajui watavipata wapi hivyo tamasha hilo litafungua ukurasa mpya juu ya watu kuweza kupata chakula hicho na sehemu gani.
Aidha, kwenye tamasha hilo kutakuwa na wapishi katika  kila kabila kupata chakula chake cha asili katika mikoa yao hiyo itakuwa ni sehemu kuwajengea utamdauni wa kupenda chakula cha asili.
Pia wananchai watapata wasaha wa huduma ya kupima afya zao na magonjwa yote bure huku pia  kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali watakaotumbuza.
Mratibu wa Tamasha hilo Bi. Zahara Michuzi  akielezea juu maandalizi ya  tamasha la vinywaji na vyakula  litakalofanyika Jumamosi katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.