Oktoba 3 ya kila mwaka dunia nzima huadhimisha siku ya makazi duniani. Na siku hii iliteuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa na kwa mara ya kwanza iliadhimishwa mwaka 1986.
Lengo kuu la kuadhimisha siku hii ni kutafakari juu  ya hali ya miji yetu na vijiji kama haki ya msingi kwa binadamu kupataa makazi ya kutosha
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa –UN Bwana Ban Ki Moon ametoa wito kwa Serikali za Kitaifa na Serikali za Mitaa pamoja na Tume za Mipango Miji duniani kote kuhakikisha inatilia mkazo swala la Ujenzi wa Makazi.
“Katika kuadhimisha siku ya Makazi Duniani, naomba kutoa wito kwa Serikali za Kitaifa na Serikali za Mitaa pamoja na Tume za Mipango Miji duniani kote kuhakikisha kuwa zinaboresha makazi ya binadamu na kufanya suala la makazi kuwa ndio jambo muhimu zaidi” amesema Bw Ban Ki Moon
“Ili kuhakikisha kila mtu anakuwa na hadhi ya kuitwa binadamu basi makazi ndio jambo la kwanza linalopaswa kutiliwa mkazo”  ameongeza Bw Ban Ki Moon
Kauli mbiu ya siku ya makazi duniani kwa mwaka 2016 ni Nyumba ni Kitovu cha Miji na azimio lingine ni kuukumbusha ulimwengu mzima kuwa una wajibu wa kuandaa mazingira mazuri kwaajili ya vizazi vijavyo.
Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC).
siku-ya-makazi
Portrait of SGKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa –UN Ban Ki Moon