Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akiangalia taarifa
zinazoingia katika mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu alipofanya ziara ya
kushtukiza katika Kituo mahiri cha kuhifadhi Kumbukumbu cha Taifa
(Internet Data Centre), kilichopo eneo la Kijitonyama jijini Dar es
salaam.
Msimamizi wa masuala ya TEHAMA
Bw. John Chorai (kulia), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), namna kifaa cha kurekodia
malipo kinavyofanya kazi wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika
Kituo mahiri cha kuhifadhi Kumbukumbu cha Taifa (Internet Data Centre),
kilichopo eneo la Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), akikagua moja ya
kifaa cha kuhifadhi Kumbukumbu katika kituo Mahiri cha Internet Data
Centre cha Taifa kilichopo eneo la Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), akifafanua
jambo kwa watumishi wa kituo Mahiri cha kuhifadhi Kumbukumbu cha Taifa
(Internet Data Centre), kilichopo eneo la Kijitonyama jijini Dar es
salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo.
Mwakilishi wa Kibiashara kutoka
Ubalozi wa Uingereza anayesimamia nchi ya Tanzania na Kenya Bw. Lord
Hollick (wa pili kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kulia) wakati
alipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia masuala ya kuboresha
miundombinu nchini. Kushoto ni Balozi wa Uingereza nchini Bi Sarah
Cookie.
………………………………………………………….
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Kampuni ya Simu Tanzania
(TTCL), kutafuta wateja wa kuhifadhi kumbukumbu zao kwenye Kituo mahiri
cha kutunzia kumbukumbu cha Taifa (Internet Data Center), jijini Dar es
Salaam
Aidha amemuagiza Mkurugenzi wa
Masoko wa kampuni hiyo kuwa mbunifu na kuanza kufuata wateja ana kwa ana
na si kusubiri wateja hao kumfuata ofisini kwake.
Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo
alipofanya ziara ya kushtukiza katika jengo hilo lililopo eneo la
Kijitonyama ambapo ameelezea umuhimu wa kufanya jitihada za haraka
kutafuta wateja hao kwa lengo la kuongeza kipato cha Taifa.
“Natoa wiki mbili kwa Mkurugenzi
wa Masoko kuhakikisha analeta wateja wa kuhifadhi kumbukumbu zao katika
kituo hiki, ikishindikana atupishe tutafute watu wanaofaa katika taaluma
hiyo”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesema kuwa Kituo
hicho kimeimarishwa kiusalama kwani kimeunganishwa na Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano hivyo wateja wataweza kuchukua taarifa zao kwa uharaka
zaidi.
Ameongeza kuwa masuala yote
yanayohusu makubaliano ya kibiashara katika kituo hicho yawekwe kwa njia
ya maandishi ili kuweza kuweka kumbukumbu sahihi na ufatiliaji
inapohitajika.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA
wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano),
Eng. Peter Mwasalyanda amemuahidi Waziri Mbarawa kutekeleza yale yote
aliyoyaagiza yafanyike ili kuboresha huduma katika kituo hicho.
Katika hatua nyingine Waziri
Prof. Mbarawa amekutana na Mwakilishi wa Kibiashara kutoka ubalozi wa
Uingereza anayesimamia nchi ya Tanzania na Kenya Bw. Lord Hollick na
kuzungumzia masuala mbalimbali ya kuboresha miundombinu nchini.
Kituo mahiri cha Internet Data Centre
ni cha kwanza kujengwa katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na
Kati na asilimia 75 zimetengwa kwa ajili ya kutunza taarifa kutoka sekta
binafsi na asilimia 25 itatunza taarifa za Serikali hivyo ni fursa mpya
kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali wenye taarifa nyingi
kuzihifadhi na kuzitumia wanapozihitaji.
0 maoni:
Chapisha Maoni