Zoezi la upimaji uzito likifanyika kupitia mpango wa AfyaKwanza.
………………………………………………………………………………………….
Mkurugenzi Raslimali Watu wa
TBL Group,Bw.David Magesse amesema mazingira ya amani na utulivu kwa
wafanyakazi katika taasisi yoyote ile yanachangia ufanisi wa kazi na
hamasa ya kujituma kwa wafanyakazi wake na alishauri kuwa kuna umuhimu
wa taasisi mbalimbali kutambua mchango wa familia za wafanyakazi wake.
Bwana Magesse aliyasema hayo
wakati akizungumzia tukio la tamasha la familia za wafanyakazi wa
kampuni ya hiyo lililofanyika jijini Dar es Salaam ambalo
liliwakutanisha wafanyakazi wa kampuni hiyo kanda ya Dar es Salaam
pamoja na familia zao ambapo walishinda na familia zao siku nzima na
kufurahi kwa pamoja.
“Sisi kama kampuni yenye
viwanda siku hii ni muhimu kwetu kwa kuwa inatukutanisha katika
mazingira ya nje ya ofisi na inatupa nafasi ya kufahamiana zaidi sisi
wenyewe na familia zetu na kujenga umoja zaidi na utaratibu huu ni wa
muhimu kwa waajiri wote kwa kuwa familia za wafanyakazi zikiwa na amani
na utulivu unawawezesha waajiriwa kufanya kazi kwa ufanisi
mkubwa”.Alisema.
Alisema TBL Group inakahikisha
katika kuongeza mori kwa wafanyakazi wake inaandaa programu mbalimbali
zinazoendana sambamba na kuhusisha familia za wafanyakazi wake “Tunao
mpango wa Afya Kwanza ambao tumekuwa tukiutekeleza kwa kuhusisha pia
familia za wafanyakazi ili kuwawezesha kuwa na afya bora”.Alisema.
Bw.Magesse alisema kuwa tamasha
la familia la Dar es Salaam ni mwendelezo wa matamasha ya familia
ambayo tayari yamefanyika katika mikoa mbalimbali ambako kampuni
imewekeza katika mikoa ya Mwanza,Mbeya,Arusha na Kilimanjaro na kuongeza
kuwa kampuni inazidi kubuni programu za kuwaweka karibu wafanyakazi
wake pia kuziweka karibu familia zao.
Nao baadhi ya wafanyakazi wa
Benki wamepongeza kitendo cha kuandaa tamasha hilo na kubainisha
kwamba ni sehemu ya kuwawezesha wafanyakazi pamoja na familia zao
kufahamiana.Wamesema tukio hilo linawawezesha wafanyakazi kupumzika na
familia zao pamoja na wafanyakazi wenzao katika mazingira tulivu na
kirafiki na kupumzika akili na kushiriki huku wakipata burudani
mbalimbali na michezo .
0 maoni:
Chapisha Maoni