Sasha Obama, bintiye Rais wa
Marekani Barack Obama, ameamua kuacha ‘starehe’ za ikulu ya White House
na kuanza kufanya kazi katika mgahawa mmoja, vyombo vya habari nchini
Marekani vinaripoti.
Binti huyo wa umri wa miaka 15
ameanza kufanya kazi ya kuwahudumia wateja katika mgahawa mmoja ulioko
Martha’s Vineyard, Massachusetts.
Sasha, ambaye anatumia jina lake
kamili, Natasha, aliandamana na maafisa sita wa ulinzi wa secret
service siku yake ya kwanza kazini, gazeti la Boston Herald linaripoti.
Familia ya Obama hutembelea eneo hilo sana wakati wa likizo.
Picha zinazosambazwa zinamuonesha bintiye huyo mdogo wa Obama akiwa amevalia sare ya hoteli akifanya kazi.
Mfanyakazi mmoja katika mgahawa
huo aliambia gazeti hilo la Herald: “Tulikuwa tunashangaa ni kwa nini
kulikuwa na watu sita walikuwa wanamsaidia msichana huyu, lakini baadaye
tukagundua alikuwa nani.”
0 maoni:
Chapisha Maoni