Kwa
kipindi cha miaka mingi iliyopita, nchi za Korea Kusini na Korea
Kaskazini zimekuwa katika vita licha ya kuwa majirani na kutokana na
historia ya vita vyao kuwa ya muda mrefu imechangia mpaka kizazi cha
sasa cha mataifa hayo kimeendelea kutokuwa na mawaelewano mazuri baina
yao.
Lakini
licha ya mahusiano ya mataifa hayo kutokuwa mazuri, michezo ya Olimpiki
ambayo inafanyika nchini Brazil inaonyesha wazi kuwa inaweza kuibua
mahusiano mapya ya mataifa hayo mawili ambayo hayapatani.
Wanamichezo
kutoka mataifa hayo mawili, Lee Eun-ju kutoka Korea Kusini na Hong
Un-jong kutoka Korea Kaskazini wameonekana wakipiga picha ya pamoja
“selfie” na wote wakiwa na nyuso za furaha jambo ambalo linatajwa kuwa
linaweza kuibua mahusiano mapya baina ya mataifa hayo.
Mwanamichezo Lee Eun-ju wa Korea Kusini akipiga picha ya pamoja “selfie” na mwanamichezo wa Korea Kaskazini, Hong Un-jong.
Mtaalam
wa siasa kutoka Marekani, Ian Bremmer amelizungumzia jambo hilo kupitia
ukurasa wake wa Twitter na kusema kuwa michezo ni njia ambayo inaweza
kuunganisha kila mtu na hilo ndiyo dhumuni la kuwepo michezo kama ya
olimpiki.
“Hii ndiyo sababu ya kufanyika Olimpiki, michezo inawaleta watu wote karibu,” alisema Bremmer.
0 maoni:
Chapisha Maoni