Michael Ray Stevenson maarufu kama Tyga (26) ni rapa wa nchini Marekani ambaye anafanya kazi zake chini ya usimamizi wa Last Kings Record lakini hapo awali alikuwa Young Money Cash Money Brothers anaweza kuingia gerezani kutokana na malimbikizo ya kodi.
Tyga alitakiwa kuwepo mahakamani siku ya Jumanne (9 August) lakini hakutokea na Jaji aliyekuwa akiendesha kesi hiyo aliamua kutoa adhabu ya kifungo kwa rapa huyo asiyeisha visa kila kukicha.
Katika kesi hiyo kuna nyaraka zinazoonesha kuwa tyga alitakiwa kulipa dola za kimarekani Elfu 16 kwa kila  mwezi na alisaini mkataba huo kwa wamiliki wa nyumba hiyo.
Tyga ambaye ameishi hapo kwa kipindi cha miezi mitatu mpaka sasa na kutokulipa hata mwezi mmoja kitendo kilichofanya apelekwe jela huku kitendo hiki kikikumbushia tukio alilolifanya tena Tyga mwaka 2012 kwa kufikishwa mahakamani Octoba 31 kwa kosa kama hilo hilo.
Licha ya hayo yote tyga atatakiwa kulipia garama za ujenzi katika sehemu zote alizoharibu kwenye eneo la nyumba hiyo, huku sehemu hizo zikiwa ni pamoja na Bafuni, Geti la kuingilia katika nyumba hiyo pamoja na vifaa vingine huku garama ya vitu vyote hivyo ikiwa ni dola za kimarekani Laki 480.
Cha kushangaza Tyga amemnunulia mpenzi wake gari aina ya Mercedes Maybach siku za hivi karibu lenye thamani ya dola laki 189 kama zawadi na akiwa ameingiza pesa za kutosha katika album yake yenye hit song kibao kama vile “Cash Money”  “1 of 1” pamoja  na “molly”
Na Derick Highiness