Kwa
mara ya kwanza nchini Tanzania na katika Historia ya music hatimaye
mashiundano ya kwanza ya kumtafuta mwanamuziki na mwimbaji wa music wa
singeli yamezinduliwa nchini mashindano hayo yakilenga kumpata msanii
mwenye uwezo wa kuimba music wa kisingeli mashindano ambayo yamepewa
jina la STAR WA SINGELI.
Mashindano
hayo ya kuimba singeli nchini Tanzania yanalenga kuibua vijana wenye
vipaji vya hali ya juu ambao wako mitaani nia ikiwa ni kuwainua na
kuwafanya kuwa wanamusic watakaotambulika ndani na nje ya Tanzania huku
pia ikiwa ni njia moja wapo ya kutengeneza ajira zenye staha kwa vijana
wa Dar es salaam.
Akizungumza
na wanahabari wakati akitangaza kuanza kwa mashindano hayo mbele ya
wanahabari Masudi Kandoro kutoka kampuni ya High Time Marketing and
Promotion ambao ndio waandaaji wakuu wa shindano hilo amesema kuwa
mashindano hayo yatafanyika katika Jiji la Dar es salaam tu na
mashindano hayo yamegawanywa katika sehemu nne ambazo ni
Kinondoni,Ilala,Temeke,na Kingamboni ambapo kila sehemu kutafanyika
mchujo kwa awamu mbili.
Ameongeza
kuwa awamu ya kwanza itakuwa katika viwanja vya wazi kila sehemu itatoa
washindani 12 kisha awamu ya pili sehemu mbili zitaungana katika
mashindano ya ndani nya ukumbi ambapo kinondoni itaungana na ilala
wakati temeke ikiungana na kigamboni.
Akizungumza
kuhusu fainali na washindi wa shindano ilo la STAR WA SINGELI amesema
kuwa fainali za mashindano hayo zitafanyika siku ya jumamosi ya tarehe
10/09/2016 katika viwanja vya Dar Live Dar es salaam kuanzia saa moja
usiku ambapo siku ya fainali atapatikana mshindi mmoja kwenye washindi
12 watakaokuwa wanawania nafasi hiyo ambapo mshindi atajinyakulia zawadi
ya million kumi.
Akizungumzia
mgawanyo wa Million Kumi hizo za mshindi wa kwanza amesema kuwa mshindi
hatapewa Kiasi icho chote bali kitagawanywa katika maeneo kadhaa
ikiwemo kupata usimamizi wa misic chini ya HIGH TIME,Kurekodi album ya
music Audio,Kufanyiwa Video tatu zenye viwango vya kimataifa,Kutangaza
Music wa mshindi ndani na nje ya mipakaya nchi pamoja na kupewa kiasi
cha Pesa Taslim.
Katika
fainali hizo zitakazofanyika Dar Live zinatarajiwa kupambwa na star wa
music huo mzee wa Hainaga Ushemeji Man Fongo na wasanii wengine wakali
ambao wanaendelea na mazunguzo kushiriki.
Wanahabari wakichukua habari wakati wa kutangazwa kwa shindano hilo la Mkali wa Singeli “Star wa Singeli”
Mratibu
wa mashindano ya Star wa Singeli, Bwana Masudi Kandoro kutoka kampuni
ya High Time Marketing and Promotion ambao ndio waandaaji wakuu wa
shindano hilo akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani) wakati wa
kutangaza shindano hilo.
0 maoni:
Chapisha Maoni