Baadhi ya wauzaji na wanunuzi na
madini ya Tanzanite walioshiriki katika mnada,Mkurugenzi wa Kampuni ya
TanzaniteOne Faisal Shahbhai,(kulia) Hussein Gonga( wa pili kulia)
mchimbaji, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya VGL Group ,Sunil Agrawal( wa
pili kushoto), na Mmoja wa Wakurugezi wa Kampuni ya TanzaniaOne, Rizwan
Ullah ( kushoto)
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel
Bendera( aliyesimama)akisoma hotuba wakati wa kumtangaza mshindi wa
zabuni ya kununua madini ya Tanzanite, katika mnada wa madini hayo
uliofanyika mkoani Arusha, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia madini wa
Wizara ya Nishati na Madini Profesa James Mdoe(wa pili kushoto),
Mkurugenzi wa kitengo cha uthaminishaji Almasi na madini ya vito,Archard
Kalugendo( kulia) na Kamishna Msaidizi wa Madini, Salim Salim( kushoto)
Mhandisi Juma Lunda( kulia)akitoa
bahasha katika sanduku maalum la kuhifadhia maombi ya zabuni za kununua
madini ya Tanzanite katika mnada.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia
Madini wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa James Mdoe,( kushoto)
akishuhudia uchambuaji wa barua za maombi ya zabuni ya kununua madini ya
Tanzanite wakati wa mnada.
Mkurugenzi wa kitengo cha
uthaminishaji Almasi na madini ya vito,Archard Kalugendo(
kulia)akitangaza washindi wa zabuni za kununua madini ya Tanzanite,mkuu
wa mkoa wa Manyara Joel Bendera( wa pili kulia) Naibu Katibu Mkuu
anayeshughulikia madini wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa James
Mdoe(wa pili kushoto).
…………………………………………………………………………………
Na Zuena Msuya Arusha
- Serikali yakusanya mbabaha wa zaidi ya milioni 331.
Serikali imekusanya mrabaha wa
zaidi ya shilingi milioni 331 katika mnada wa madini ya Tanzanite
yaliouzwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 7.56 kutoka kampuni mbili za
uchimbaji madini hayo katika eneo la Mirerani mkoani Manyara.
Akitangaza washindi wa zabuni za
kununua madini ya Tanzanite mkoani Arusha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Manyara, Joel Bendera, Mkurugenzi wa kitengo uthaminishaji Almas na
madini ya vito(TANSORT), Ardhard Kalugendo alisema kuwa katika mnada huo
kampuni tano zilijitokeza, mbili kati ya hizo ziliuza madini yake kwa
wanunuzi mbalimbali; Kampuni tatu hazikuweza kuuza kutokana na
kutokubalina bei na wanunuzi.
Kalugendo alifafanua kuwa mnada huo ulifanyika kwa njia ya uwazi na kushirikisha wafanyabiashara wa ndani na nje ya Tanzania.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Manyara, Joel Bendera alisema kuwa mnada huo umeiwezesha Serikali kupata
mrabaha pamoja na kuzuia utoroswaji wa madini hayo nje ya nchi uliokuwa
ukiikosesha Serikali mapato yake kwa maendeleo ya taifa.
Katika hatua nyingine Bendera
aliwatoa hofu wachimbaji wa madini ya Tanzanite katika migodi ya
Mirerani mkoani Manyara kuwa kwa Serikali imeimarisha ulinzi kwa usalama
pamoja na mali zao; Pia wafanyabiara wa Tanzanite watoe ushirikiano kwa
vyombo vya usalama pale wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa amani.
Aidha aliwasihi wanunuzi na
wachimbaji wa Tanzanite kufuata sheria na taratibu za uchimbaji na
ununuzi ili kuhakikisha kuwa madini hayo adhimu yanayopatikana nchini
tanzania pekee duniani yanawanufaisha watanzania wote.
Naye Naibu Katibu Mkuu
anayeshughulikia Madini wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa James
Mdoe alisema kuwa pamoja na manufaa yaliopatikana katika mnada huo,
Serikali itaendelea kuboresha mnada huo kwa kuongeza muda zaidi ili
kutoa fursa kwa kila mfanyabiasha wa Tanzanite kushiriki; Vilevile
kuwepo na majadiliano zaidi kati ya wauzaji na wanunuzi wa madini ya
Tanzanite ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Profesa Mdoe aliongeza kuwa lengo
la Serikali katika mnada huo ni kuwawezesha wafanyabiashara wa Tanzanite
kupata matokeo chanya na yenye tija katika shughuli zao, pia Taifa
linufaike kutokana na matokeo hayo kwa njia mbalimbali.
Mmoja wa wafanyabiashara ya madini
ya Tanzanite, ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzaniteone Faisal
Shuhbhai aliipongeza Serikali kwa kuweka utaratibu huo ambao ni wa
kwanza kufanyika nchini kwakuwa utawawezesha wafanyabiashara hao kufanya
shughuli zao kwa ufanisi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Faisal alisema kuwa utaratibu wa
mnada utawawezesha wafanyabiashara wa Tanzanite waliokuwa wakikwepa
kodi, kulipa mirabaha kwa wakati baada ya kuwepo kwa mpango huo ambao
haukuwepo hapo awali; Aidha utawasaidia wafanyabiara kupata bei elekezi
inayoendana na soko la dunia na hivyo kuacha kutorosha madini ya
Tanzanite nje ya Tanzania kwa madai ya kutafuta masoko.
0 maoni:
Chapisha Maoni