Postedy by Esta Malibiche on August 8.2016 in KITAIFA with No comment
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe
Miraji Jumanne Mtaturu akisalimia na Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu-
Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde (Mb) mara baada ya kuwasili
katika uwanja wa Maonesho ya wakulima Nane nane kwa ajili ya kufunga
maonesho hayo
Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu-
Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde (Mb) akisikiliza kwa makini
maelekezo ya namna ya kuchakata mihogo kutoka kwa mkulima wa zao hilo
tangu mwaka 1980 kutoka Kijiji cha Nzuguni Josiah Malogo Ndoya
Mhe Mavunde (Mb) akisikiliza kwa makini namna ya kulima mahindi kwa mbinu bora na za kisasa ili kuwa na mavuno yenye tija
Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu-
Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde (Mb) akisikiliza maelekezo
katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kuhusu umuhimu wa
matumizi ya dawa katika kilimo cha kisasa
Mhe Mavunde alipotembelea banda la ushonaji la Jeshi la kujenga Taifa JKT katika Maonesho ya Nane nane kabla ya kuyafunga rasmi
Mhe Mavunde alipotembelea banda la
maonesho ya wanyama aina ya mbuzi, Ng’ombe na Kondoo la kampuni ya
Ranchi za taifa (NARCO LTD)
007 Naibu waziri ofisi ya Waziri
Mkuu- Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde (Mb) akipokea zawadi
ya mboga za majani kutoka kwa vijana wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT)
mara baada ya kutembelea banda hilo
008 Mhe Mavunde alipotembelea banda la Maonesho ya kilimo cha Vitunguu
009 Mhe Mavunde akisalimiana na
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma marabaada ya
kutembelea banda la maonesho la Wilaya hiyo
Mhe Mavunde akitazama ubora wa matrekta yaliyofikishwa katika Maonesho ya wakulima ya Nanen nane
0011 Naibu waziri ofisi ya Waziri
Mkuu- Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde (Mb) akiwa katika
picha ya pamoja na viongozi mbalimbali walioshiriki katika maonesho ya
Nane nane katika uwanja wa Nzuguni Kanda ya kati Dodoma
……………………………………………………………………………………………….
Na Mathias Canal, Dodoma
Maonesho na Mashindano ya mifugo
Kitaifa sanjari na Maonesho ya Kilimo yametoa changamoto ya kuleta
mapinduzi katika Ufugaji, Uvuvi, na Kilimo na kutoa ajira hususani kwa
vijana kuwaongezea zaidi kipato na kuondoa umasikini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde wakati
akifunga maonesho ya wakulima Nane nane Kanda ya Kati Dodoma yaliyokuwa
yanafanyika katika uwanja wa Nzuguni kwa kauli mbiu ya “Kilimo, Mifugo
na Uvuvi ni nguzo ya Maendeleo, Kijana shiriki kikamilifu (Hapa Kazi
Tu).
Amesema kwa kuwa serikali ya awamu
ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais John Pombe Magufuli inatekeleza azma
ya kuhamishia makao makuu mjini Dodoma ameishauri Wizara ya Kilimo,
Mifugo, na Uvuvi na ile ya Biashara na masoko kuangalia uwezekano wa
kuanzisha rasmi maonesho ya Kilimo, Mifugo, na Uvuvi ya Kimataifa
(International Agriculture Trade Fair) katika uwanja wa Nzuguni ambao
ndio uwanja wenye eneo kubwa kwa maonesho ya Kilimo hapa nchini.
Aidha ametoa wito kwa Wizara,
taasisi/Makampuni ya umma na binafsi, Mabenki na wadau wote wa kilimo na
mifugo kuendelea kuwasaidia wakulima na wafugaji hapa nchini ili
kuongeza uzalishaji kuwezesha upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya
viwanda vinavyokusudiwa kuanzishwa.
“Naomba niwaambie wakulima na
wafugaji wetu kuwa maonesho ninayoyafunga hii leo ni muafaka na fursa
nzuri kwao hususani vijana kwenda kuanza mara moja kutumia mlichojifunza
na kuleta mapinduzi yenye maendeleo chanya yanayotarajiwa kiuchumi,
hivyo napenda kuchukua nafasi hii kuzikumbusha Halmashauri za serikali
za mitaa zote kuwahamasisha wakulima, Wafugaji na wadau wengine kutumia
teknolojia zilizooneshwa hapa kuongeza ufanisi wao katika Kilimo, Mifugo
na Uvuvi” Alisema Mavunde
Naibu waziri huyo pia ametoa
zawadi kwa washindi katika Halmashauri za Mkoa wa Dodoma na Singida,
Wizara za serikali, Taasisi za uzalishaji wa serikali, Makampuni ya
pembejeo za Kilimo na Mifugo, Makampuni ya zana za Kilimo na Mifugo,
Taasisi za serikali na Mashirika ya Umma, Taasisi za fedha na Mabenki,
Taaisisi za mafunzo na utafiti, Taaisisi zisizo za kiserikali (NGOs na
CBOs), Taasisi za mawasiliano ya kibiashara, Mamlaka za udhibiti, Vyombo
vya habari, na Kampuni za nishati mbadala kwa kufanya vizuri katika
maonesho hayo.
Pia zawadi hizo zimetolewa pia kwa
watu wenye mashamba makubwa ya ufugaji ng’ombe wa maziwa, Wafugaji
wadogo wa ng’ombe wa nyama, Wafugaji bora, na Wakulima bora.
Sambamba na hao pia Jeshi la
Kujenga Taifa JKT limeibuka kidedea kwa ushindi wa jumla likifuatiwa na
Jeshi la Magereza ambapo nafasi ya tatu imechukuliwa na Wizara ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvu.
Akitoa maelezo ya awali kuhusu
maonesho hayo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu amesema kuwa Malengo ya maonesho hayo ni utoaji elimu ya
matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa wadau wengi kwa muda mfupi lakini
pia wadau kujionea na kujifunza huduma zitolewazo na serikali, mashirika
ya umma na binafsi.
Mtaturu alisema kuwa mpaka tarehe 7
hapo jana jumla ya watu waliokuwa wametembelea inakadiriwa kuwa 40,000
huku matarajio ya siku ya ufungaji ikitarajiwa kuongezeka watu 12,000 na
kufikia idadi ya watu 52,000.
Dc Mtaturu amesema kuwa
Teknolojia/Bidhaa zilizooneshwa ni pamoja na zana za Kilimo, Mbegu bora
za mazao mbalimbali, Uzalishaji wa mazao katika mazingira
yaliyodhibitiwa (JKT Kondoa) Taasisi za kitafiti ambazo zimeonyesha
teknolojia mbalimbali za kuongeza tija zenye ukinzani dhidi ya magonjwa
mbalimbali, Utengenezaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo,
Uboreshaji wa viasilu ili kupata mifugo na mazao ya kilimo
yanayostahimili hali ya hewa ya kanda ya kati na udhibiti wa magonjwa.
Pia uzalishaji bora wa mazao ya
nafaka, ubunifu wa teknolojia rahisi za kutotoa mayai, Kuongeza thamani
mazao ya mifugo, Makampuni ya mawasiliano, Taasisis za elimu zimeonyesha
ubunifu wa kumsaidia mfugaji, Tiba za asili, Wasindikaji wakubwa na
wadogo wa mazao ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Asali, na Nta.
Akitoa salamu za shukrani kwa
niaba ya waandaaji wa Maonesho hayo Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias
Tarimo amemshukuru mgeni rasmi Antony P. Mavunde kwa kuitikia wito wa
kufunga maonesho hayo ambapo pia ameishukuru Benki kuu ya Tanzania
(BOT), Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Halmashauri ya Wilaya ya Chemba,
LAPF, Mkuu wa Mkoa wa Singida na Chuo kikuu cha Dodoma kwa uwakilishi
na uchangiaji kwa ajili ya maonesho hayo.
Maonesho ya sikukuu ya wakulima
Nanenane Kanda ya kati Dodoma yaliyohusisha shughuli za wakulima,
wafugaji wa mifugo, wafugaji wa nyuki, wavuvi, wanamazingira,
wasindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na mifugo, wizara
taasisi/makampuni ya umma, makampuni binafsi, mabenki, Taasisi za umma
na binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali yalifunguliwa tarehe 03
Agosti 2016 na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe.
0 maoni:
Chapisha Maoni