Postedy by Esta Malibiche on August 12.2016 in MICHEZO with no comment
Mchezaji wa Timu ya Tanzania
Mtumwa JUma akipambana na walinzi wa Timu ya Uganda wakati wa michezo
ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki kat.ika uwanja wa Amahoro Kigali
Rwanda ambapo Tanzania ilishinda 24-23(\Picha na Selemani Semunyu).
Mshambuiliaji wa Timu ya Tanzania
Ally Hamisi (Mwenye jezi namba 11) akipambana na walinzi wa Timu ya
Uganda wakati wa michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki
kat.ika uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo Tanzania ilishinda
24-23(\Picha na Selemani Semunyu)
Mshambuiliaji wa Timu ya Tanzania
Ally Hamisi (Mwenye Mpira ) akitafuta namna ya kuwatoka walinzi wa
Timu ya Uganda wakati wa michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika
Mashariki kat.ika uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo Tanzania
ilishinda 24-23(Picha na Selemani Semunyu)
Baadhi ya mashabiki wa Timu ya
Tanzania Wakishangilia wakati Timu yao ikipambana na Uganda wakati wa
michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki kat.ika uwanja wa
Amahoro Kigali Rwanda ambapo Tanzania ilishinda 24-23(\Picha na Selemani
Semunyu)
…………………………………………………………………………………………..
Na Selemani Semunyu JWTZ
Timu ya mpira wa Mikono ya Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania imefanikiwa kurejesha nguvu yake
baada ya kuifunga Timu ya Jeshi la Uganda UPDF kwa 24-23 katika Mchezo
wa Pili wa Timu hiyo uliokuwa na ushindani mkali baina ya Timu hizo.
JWTZ imeifunga UPDF Timu zote
zilianza Mchezo taratibu huku wakijaribu kusomana wachezaji wa timu hizo
hali il;iyokuwa ikibadioli mchezo huo katika kila dakika inayomalizika
huku tanzani awakionekana kuwazidi wenzao wa Uganda.
Hadi Nusu ya Kwanza ya Mchezo
huo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro ilimalizika huku Timu ya
Tanzani ilikuwa ikiongoza kwa magoli 12 -9 dhidi ya Uganda ambao
walionekana kupoteana katika kipindi hicho chwa kwanza.
Kipindi cha pili Uganda
waliingia kwa Nguvu huku wakionyesha kufaidika na Kipindi cha mapunziko
kwani walifanikiwa kupunguza idadi ya Tofauti ya magoli na kuibana
Tanzania kutokuwa na tofauti kubwa na hatimaye kufanikiwa kutoka
uwanjani wakiwa wamefungana kwa tofauti ya Goli Moja.
Nahodha wa Timu ya Tanzania
Sedrick Damiano alisema kipingon walichopata katika Mchezo wa kwanza
kutoka kwa Rwanda kimewafanya kubadilika na kurekebisha makosa
yaliyojitopkeza sambamba kuwa makini na Waamuzi.
Pia Alisema ni mategemeo yake
ushindi huu utakuwa salamu tosha kwa Wapinzani wao Kenya ambao
watakutana nao katika mchezo unaotarajiwa kufanyika Agosti 14 katika
uwanja wa Amahoro.
Kwa Upande wake mkurugenzi wa
Michezo wa JWTZ Brigedia Jenerali Martin Busungu alisema ushindi huo
umewapa nguvu ya kuhakikisha wanashinda katika michezo iliyosalia.
Katika Mchezo Mwingine katika
Mpira wa pete Tanzania inatarajiwa kukutana na Wenyeji Rwanda wakati
katika Mpira wa Miguu Tanzania inatarajia Kukutana na Kenya katika
Uwanja wa Kigali Nyamirambo.
0 maoni:
Chapisha Maoni