Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela ameshiriki uzinduzi wa Kanisa la Efatha Mlima wa Sayuni katika mtaa wa Lugalo B Wilolesi Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa.
Akitoa salamu za serikali alisema maarifa huyapati kwa kuomba tu bali ni ile hali yako ya uelewa na ukafanya unavyo elewa huku ukimtegemea Mungu. akaendelea
Tunapokataa kukaa na Mungu, Mungu naye hutuacha nasi tutaendelea kutumia akili zetu, akili zetu bila Mungu ni kazi bure"
DcKasesela alimuomba Mtumishi wa Mungu Josephat Mwingira kuuombea mkoa wa Iringa ili uondokane na dhambi zinazowatenganisha wananchi wake na Mungu kwa kufanya vitendo visivyofaa katika jamii vikiwemo ubakaji, ushirikina,Uvivu na Wizi
Naye Nabii Mwingiraawali akifungua Ibada alisema sasa Tanzania ipo katika mabadiliko ya majira ya Mungu
Alisema Elimu iliyopo itabadilika na kuendana na mfumo wa Mungu ili liondokane na elimu ya kitumwa ambapo kila mwanafunzi amalizapo shule asihangaike kutafuta kazi,bali aajiliwe kulingana na Elimu aliyoipata.
" Ukimuona mtu amemaliza shule anahangaika mitaaani na barua za kuomba kazi ujue huyo hajaelimika bali kaenda shule" alisema
0 maoni:
Chapisha Maoni