Wafanyakazi
wa kampuni ya TBL Group na wanajamii wote wameaswa kuzingatia kanuni za
usalama na kuzitekeleza wakati wote ili kuepuka uwezekano wa kupata
majanga ambayo yanaweza kuepukika .
Wito
huo umetolewa na Meneja anayesimamia mazingira ya sehemu za kazi na
Usalama wa kiwanda cha TBL Group ,Renatus Nyanda wakati akihojiwa
kuhusiana na maadhimisho ya Siku ya Usalama Kazini Duniani ambayo
imeadhimishwa na kampuni hiyo kwa kushirikisha wafanyakazi wake wote .
Nyanda
alisema kuwa linapozungumziwa suala la usalama mahali pa kazi wengi
wamekuwa wakidhani kuwa unapaswa kuzingatia kanuni za usalama unapokuwa
kazini tu,dhana ambayo alidai kuwa ni potofu kwa kuwa Usalama unapaswa
kuzingatia wakati wote na mahali popote na kuwa suala la usalama
linamhusu kila mtu awe mfanyakazi wa ofisini, kiwandani, mkulima,
mfanyabiashara na shughuli nyinginezo.
Mkuu
wa kitengo cha elimu kwa Umma kitengo cha Usalama barabarani makao
makuu ya Polisi ASP,Abel Swai akitoa mada kwa wafanyakaziwa kampuni ya
TBL jijini Dar es Salaam wakati wa semina ya masuala ya usalama wakati
kuadhimisha Siku ya Afya na Usalama Duniani.Semina hiyo ilifanyika
kiwanda cha TBL cha Ilala.
Alisema kampuni ya TBL Group
imekuwa ikilipa kipaumbele suala la usalama kwa wafanyakazi wake ambapo
tayari imefanikiwa kupunguza matukio ya ajali kazini kwa wafanyakazi
wake kutokana na utekelezaji wa mpango wa tahadhari za kiafya na usalama
wa kampuni mama ya SABMiller ambao umefanyiwa utafiti wa kina na wenye
kutoa maelekezo ya kuepusha ajali sehemu kazini na maeneo mengine mbali
na kazini.
Alisema elimu hii ya tahadhari na usalama ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara na kutekelezwa kwa vitendo haiwasaidii wafanyakazi wanapokuwa kazini tu bali hata wawapo majumbani kwao au sehemu yoyote nyingine wakiitumia itawasaidia kuwaepusha na majanga mbalimbali ambayo yamekuwa yakijitokeza katika shughuli za maisha ya kila siku.
“Programu hii inayojulikana kama Safety around Bevarage inafundisha masuala mengi kuhusiana na usalama kazini ambapo tangu ianze kutekelezwa na kampuni ya TBL Group imeanza kuonyesha mafanikio katika ofisi na viwanda vyake vyote kwa kuwa ni nadra matukio ya ajali kujitokeza kwa wafanyakazi na wageni wanaotembelea kampuni na taasisi nyingi zinavutiwa kuja kwenye kampuni yetu kujifunza masuala ya usalama”.Alisema

wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL wakisikiliza mada wakati wa semina ya
usalama kazini wakati wa maadhimisho ya siku ya Afya na Usalama Duniani.
Katika kuadhimisha siku hii
wafanyakazi walishiriki semina zinazohusiana na masuala ya usalama
zilizotolewa na serikali kupitia jeshi la polisi kitengo cha usalama
barabarani pia wataalamu wa masuala ya bima na Afya ya jamii walitoa
mada kuhusiana na umuhimu wa kuwa na bima.
Maadhimisho ya siku ya Usalama kazini Duniani huadhimishwa Aprili 28 kila mwaka ambapo kampeni za kuhamasisha usalama mahali pa kazi hufanywa na taasisi mbalimbali duniani kote.
Maadhimisho ya siku ya Usalama kazini Duniani huadhimishwa Aprili 28 kila mwaka ambapo kampeni za kuhamasisha usalama mahali pa kazi hufanywa na taasisi mbalimbali duniani kote.
Mmoja
wa wafanyakazi wa TBL akiuliza swali wakati wa semina ya usalama kazini
wakati wa maadhimisho ya siku ya Afya na Usalama Duniani iliyofanyika
kiwanda cha ilala jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu
wa masuala ya afya na jamii Lilian Msaki,akitoa elimu kwa wafanyakazi
wa TBL wakati wa semina ya usalama kazini wakati wa maadhimisho ya siku
ya Afya na Usalama Duniani iliyofanyika kiwanda cha ilala jijini Dar es
Salaam.
Maofisa
wa Jeshi la Polisi na TBL wakibadilisha mawazo muda mfupi baada ya
kumalizika kwa semina semina ya usalama kazini wakati wa maadhimisho ya
siku ya Afya na Usalama Duniani iliyofanyika kiwanda cha ilala jijini
Dar es Salaam.