Kata ya Bulamata iliyoko katika tarafa ya Mishamo Wilayani Tanganyika mkoa wa Katavi imeanza Ujenzi wa Shule ya Sekondari Bulamata itakayokuwa ya kutwa na bweni itakayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 3 na milioni 840 ikiwa ni mpango wa miaka kumi ijayo.
Hayo yamebainishwa na Diwani wa kata hiyo Nicas Nibengo wakati Mbunge wa viti maalumu mkoa wa katavi,  Mheshimwa Anna Lupembe alipotembelea katika kata hiyo na kushuhudia Nguvu kubwa ya wananchi ikishiriki katika Kujitoa kujenga shule kwa ajili ya watoto wao.
Pia Mheshimiwa diwani amesewapo katika harakati za ujenzi wa shule ya msingi ya pili  katika kijiji cha busongola  ili kuwezesha watoto kupata elimu bila msongamano.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Busongola ambacho kipo ndani ya kata hiyo ya Bulamata Felician Odasi amesema watoto wao watanufaika na Elimu baada ya kukamilika kwa ujenzi huo kwani wamekuwa wakipata taabu kwa muda mrefu kutokana na kukosekana kwa shule ya sekondari katika kata yao.
Aidha nae  Mbunge wa viti maalumu mkoa wa katavi  Mh.Anna Lupembe akashiriki katika zoezi la kusogeza tofali na mawe hukuamempongeza diwani kwa jitihada zake mahusui kuwezesha kuibua mradi wa ujenzi wa sekondari huku akiahidi kumpa ushirikiano kwa asilimia mia moja.
img_3161Mh. Anna Lupembe Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Katavi akikagua eneo hilo litakalojengwa shule..mawe na tofali vikiwa pembeni ya msingi tayari kwa ajili ya ujenzi.
img_3160Baaadhi ya Wananchi wakiendelea na ujenzi kwa kusaidiana na mafundi  wao.