Posted by Esta Malibiche on Oct7.2016 in UTAMADUNI
.
Naibu Spika, Dk Tulia Ackson akisaidiana na Wabunge kumvalisha shuka la heshima ya Wanyakyusa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
WATANZANIA
wametakiwa kutumia sanaa na utamaduni kwa ajili ya kutangaza amani na
mshikamano ikiwa ni pamoja na kuenzi mila na desturi ambazo zilianza
kupotea.
Wito
huo ulitolewa na Balozi wa Kenya nchini Tanzania Chirau Mwakwere
alipokuwa akitoa salam katika Tamasha la Ngoma za jadi lililoandaliwa na
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Akson
Mwansasu linalofanyika kwa siku mbili katika viwanja vya Tandale Tukuyu
wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya.
Balozi
alisema Utamaduni pia unaweza kutumika katika kujenga mahusiano mazuri
baina ya nchi na nchi ikiwa ni pamoja na kukutanisha watu wa aina mbali
mbali kwa pamoja.
Akifungua
Tamasha hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla alimpongeza Naibu
Spika kwa ubunifu na kuanzisha wazo la kushindanisha ngoma za jadi za
Mbeya jambo alilosema litasaidia kufufua utamaduni uliofifia.
Alisema
kupitia utamaduni huo kutangaza mila na desturi za wazawa, kutangaza
vivutio vya utalii, kuelimisha na kufundisha jamii, kutengeneza ajira
kwa vijana pamoja na kuchochea uzalendo kwa Taifa pamoja na kukuza
Uchumi.
Aliongeza
kuwa zoezi hilo linapaswa kuwa endelevu kwa kufanywa Mkoa wote pamoja
na Taifa kwa ujumla ili vizazi vilivyopo na vijavyo viweze kukumbushwa
utamaduni wa makabila yao.
Kwa
upande wake Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson Mwansasu alisema mashindano
hayo yalianzia kwenye ngazi ya kijiji katika Halmashauri za Kyela,
Rungwe na Busokelo ambapo walipatikana washindi na kushindanahadi ngazi
za Wilaya ambao wanashindana kumpata mshindi mmoja atakaye ziwakilisha
Wilaya za Kyela na Rungwe kwenda mkoani Dodoma.
Alisema
katika mashindano hayo jumla ya vikundi 35 ambavyo 16 vinatoka Rungwe
na 19 Wilaya za Kyela vinashindana katika aina 9 za ngoma za Jadi za
Kabila la Wanyakyusa.
Aidha
katika Tamasha hilo ambalo litafanyika kwa sku mbili kati ya Oktoba 7
na 8, mwaka huu limehudhuriwa na Wabunge zaidi ya 12 akiwepo Naibu
Waziri wa Elimu Mhandisi Stellah Manyanya ambapo pia linatarajiwa
kufungwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye
|
Mbunge viti maalum Mkoa wa Mbeya, Dk Mary Mwanjelwa akizungumza katika tamasha huku akiwa na waunge wengine wa Mkoa wa Mbeya |
Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa akimvalisha shuka mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akiwa meza kuu pamoja na viongozi wengine wakifuatilia mashindano ya ngoma za asili |
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia mashindano ya ngoma za jadi |
Balozi wa Kenya nchini Tanzania akitoa salam katika Tamasha |
Wabunge mbalimbali wakicheza na Naibu Spika |
Naibu Spika akiongelea lengo la kuandaa tamasha hilo la ngoma za jadi |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akitoa hotuba ya ufunguzi wa Tamasha la ngoma za Jadi |
Naibu Spika akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla |
0 maoni:
Chapisha Maoni