Usiku wa kuamkia jumamosi kumechezwa michezo ya kutafuta nafasi ya kushiriki nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia 2018, katika michezo yote iliyopigwa, timu iliyopata ushindi mkubwa ilikuwa ni Ureno ambayo iliibuka na ushindi wa goli 6-0 dhidi ya Andorra.
Katika ushindi huo, nahodha wa Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo alifunga magoli manne na mengine mawili yakifungwa na Joao Cancelo na Andre Silva.
Pia Andorra walimaliza mchezo huo wakiwa nusu baada ya wachezaji wake wawili, Jordi Rubio na Marc Rebes kuonyeshwa kadi nyekundu.
Baada ya mchezo kumalizika Ronaldo alizungumzia ushindi walioupata na magoli manne aliyofunga yaliyoisaidia Ureno kupata alama tatu na kushika nafasi ya tatu katika Kundi B ambalo linaongozwa na Switzerland.
“Tulijua kuwa goli la kwanza lilikuwa na umuhimu sana kwetu ambalo lingetuwezesha kuwa mbele katika timu ambayo ilikuwa na wachezaji 11 nyumba ya mpira,
“Najua nina umuhimu kama wachezaji wengine. Nimejitoa kwa kila kitu kwa ajili ya timu yangu ya taifa, najihisi nimetumika na nina furaha baada ya kurejea kutoka katika majeruhi niliyoyapata katika mashindano ya Ulaya,” alisema Ronaldo.