Waziri wa elimu nchini Sweden amejiuzulu wadhifa wake baada ya kupatikana akiendesha gari akiwa mlevi.
Bi Aida
Hadzialic, ambaye amekuwa waziri wa elimu ya sekondari na elimu ya watu
wazima, amejiuzulu baada ya kukamatwa na polisi Malmo.
Kwenye
taarifa iliyoonyesha hisia nyingi, Bi Hadzialic , ambaye ndiye mtu
mchanga zaidi kuwahi kuteuliwa waziri nchini humo, amesema sharti
awajibike kwa alichosema ni kosa kubwa zaidi alilowahi kulifanya
maishani mwake.
Alipimwa na kugunduliwa kwamba alikuwa tu amepitisha kidogo kipimo kinachoruhusiwa cha unywaji pombe.
Sweden huwa na sheria kali sana za kuzuia uendeshaji gari mtu akiwa amelewa.
Bi Hadzialic,
aliyehamia Sweden kama mkimbizi Mwislamu kutoka Bosnia Herzegovina
akiwa mdogo, amesema alikuwa amekunywa gilasi mbili pekee za mvinyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni