Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo NAPE NNAUYE, amelifungia Gazeti la Mseto kwa Miezi 36 kutokana
na kuchapisha Habari za Uongo na kugushi kwa kutumia nyaraka mbalimbali za
Serikali.
Uamuzi huo wa kulifungia Gazeti hilo umetolewa kwa Tangazo
la Serikali Namba 242 lilitolewa jana kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka
1976 Sura ya 229, Kifungu 25(1).
Waziri NAPE ameeleza kuwa Kifungu hicho kinampa Mamlaka Waziri
kuchukua uamuzi wa kufungia Gazeti kutokana na mwenendo wa uandishi wa Gazeti
hilo wa kuandika na kuchapisha habari za uongo na Kugushi kwa kutumia nyaraka
mbalimbali za Serikali.
Amefafanua kuwa Serikali kwa masikitiko makubwa imelazimika
kilifungia Gazeti la Mseto kutokana na mwenendo wa uandishi wa kuandika na
kuchapisha habari za uongo na kugushi.
Ameongeza kuwa Serikali ya Tanzania imeridhia mikataba
mbalimbali ya Kimataifa inayoanisha Uhuru wa Habari na mipaka ya Habari ikiwemo
tamko la Haki za Binaadamu la mwaka 1948.
Gazeti la Mseto limezuiwa kuchapishwa katika njia nyingine
yeyote ikiwemo mitandao kwa mujibu wa Sheria ya MawasiliMsikilize Waziri Nape hapa
0 maoni:
Chapisha Maoni