Posted by Esta Malibiche on FEB 16,2017 IN NEWS
Mgeni
rasmi akiwa waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage
wa tatu kushoto,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kiwanga cha
utengenezaji wa viungo,Vegata Podravka Ltd,kilichojengwa kwa gharama ya
shilingi bilioni 16,Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Bagamoyo,Mh.Shukuru
Kawambwa na kulia ni Makamu wa Rais wa Kampuni ya Podravka Group kutoka
nchini Croati,Bi.Olivia Jakupec.
waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijagea akipata
maelekezo mbalimbali kuhusiana na baadhi ya bidhaa ambazo ziko tayari
kutoka kwa Makamu wa Rais wa Kampuni ya Podravka Group kutoka nchini
Croati,Bi.Olivia Jakupec.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kiwanda cha Vegeta Podravka Ltd,Bw-Tanzania,.Davor Svar
akizungumza kwa ufupi wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho cha viungo
mbalimbali,jana mjini Bagamoyo,huku mgeni rasmi akiwa waziri wa
Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage.
Davor
alisema kuwa wameamua kuwekeza nchini Tanzania kwa sababu imeonekana ni
kiungo muhimu katika mambo ya uwekezaji hasa kutokana na eneo lake,
miundo mbinu yake,ukuaji wake wa kiuchumi na pia kuwa kiungo muhimu kwa
kuwa mwanachama hai wa nchi za Afrika Mashariki na Kati,kufuatia vigezo
hivyo,hurahisisha mambo ya kibiashara kufanyika kwa urahisi zaidi.
Davor
alisema kuwa kufuatia kuanzishwa kwa kiwanda hicho,kimefanikiwa kutoa
ajira za kazi zaidi ya 200 katika Wilaya ya Bagamoyo ikiwemo kazi ya
uuzaji na usambaji wa bidhaa za kiwanda hicho.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kiwanda cha Vegeta Podravka Ltd-Tanzania,Davor Svar
akifafanua jambo kwa Mgeni rasmi,Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji
Mh.Charles Mwijage,kabla ya hafla fupi ya uzinduzi wa kiwanda
hicho,uliofanyika mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani na kuhudhuriwa na wadau
mbalimbali.
Makamu
wa Rais wa Kampuni ya Podravka Group kutoka nchini Croatia ,ambayo ni
kampuni mama ya Vegeta Tanzania,Bi.Olivia Jakupec akizungumza mbele ya
wageni waalikwa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho cha
utengenezaji wa viungo mbalimbali,mjini Bagamoyo mkoani mkoani Pwani.
Olivia
alisema kuwa wao kama wawekezaji wametembea nchi kadhaa za Afrika
ikiwemo Uganda,Kenya,Burundi,Zambia,Rwanda,Sudani Congo,Afrika Kusini na
nyinginezo,lakini wakabaini Tanzania ndio mahali sahihi kwa
uwekezaji."Hivyo tukafanya utafiti,tukabaini eneo la Bagamoyo linafaa
kujengwa kiwanda cha aina hiyo,hivyo tukaamua kujenga kiwanda ndani ya
mwaka mmoja na nusu,ambacho kimetumia kiasi cha shilingi bilioni 16
mpaka kukamilika.
"Tunaishukuru
Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Waziri wa
Viwanda Mh.Charles Mwijage,Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na
wengineo kwa ujumla, kwa kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji,kiasi
kwamba hata nasi tukaiona furasa hiyo na tukachukua hatua ya kuwekeza
kiwanda hiki hapa nchini",alisema Olivia.
Baadhi
ya Wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa
kiwanda cha Viungo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijagea
akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla
ya uzinduzi wa kiwanda hicho wilayani Bagamoyo,Pwani.Waziri Mwijage
alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano imeamua kujenga Uchumi wa
Viwanda,ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya Watu.
"Tanzania
sasa tunajenga viwanda na si Tanzania ya viwanda inawezekana,hiyo
ilikuwa kauli mbiu ya zamani,kwa hiyo sasa tunajenga viwanda,mwenye
macho haambiwi Tazama"alifafanua Waziri Mwijage.Waziri Mwijage
amewashuruku wawekezaji hao kwa kuamua kuja kuwekeza nchini
Tanzania,ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais wa awamu ya tano ,Dkt
John Pombe Magufuli katika kuhakikisha Uchumi wa Viwanda unakwenda kwa
kasi na kufanikiwa.
Waziri
wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage akipeana mkono na
Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Vegeta Podravka
Ltd,Bw-Tanzania,.Davor Svar mara baada ya kusoma hotuba yake
iliyowahamasisha wakati wa Wilaya ya Bagamoyo kuchangamkia fursa
mbalimbali zitokazo na ujenzi wa viwanda vya aina mbalimbali
vinavyoendelea kujengwa wilyani humo mkoani Pwani.
Sehemu ya meza kuuu
Wageni waalikwa kutoka kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),wakifautilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri
Baadhi ya wageni waalkwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla hiyo
Makamu
wa Rais wa Kampuni ya Podravka Group kutoka nchini Croatia ,ambayo ni
kampuni mama ya Vegeta Tanzania,Bi.Olivia Jakupec akimkabidhi Waziri wa
Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage cheti cha heshima ya
ushiriki wake mkubwa katika uzinduzi wa kiwanda hicho
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Podravka Group kutoka nchini Croatia
,ambayo ni kampuni mama ya Vegeta Tanzania,Bi.Olivia Jakupec akimkabidhi
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage cheti cha
heshima ya ushiriki wake mkubwa katika uzinduzi wa kiwanda hicho.Pichani
kati ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Vegeta Podravka
Ltd-Tanzania,Davor Svar.
picha ya pamoja
Picha pamoja
Baadhi
ya Wawakilishi kutoka Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) wakipewa maelezo
mafupi namna ya bidhaa hizo zinavyotengenezwa kiwandani hapo
Baadhi ya wafanyakazi wakiendelea na usindikaji wa viungo kiwandani humo
0 maoni:
Chapisha Maoni