Alhamisi, 11 Agosti 2016

MBUNGE WA CHALINZE RIDHIWANI KIKWETE AKUTANA NA KINA MAMA WA JAMII YA WaFUGAJI


Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,wa pili kutoka kulia,akiangalia ngoma ya asili ya wakina Mama wa jamii ya wafugaji,alipofika kwa ajili ya kusikiliza kero za kina Mama hao katika utaratibu alijiwekea wa kusikiliza kero za wananchi wa jimbo hilo.
Baadhi ya kina Mama wakicheza mbele ya Mbunge wa mara baada ya kumpoe.

Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amekutana na kina Mama jamii ya wafugaji katika eneo la Chamakweza na kusikiliza kero za kina Mama hao katika utaratibu wa kusikiliza kero zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo.

Akizungumza na kina Mama hao Mbunge huyo,amesema kuwa atasaidia kutatua kero zilizopo katika eneo hilo,na kutaja baadhi ya kero zinazowakabili,ni ukosefu wa Zahanati ambapo ujenzi umeanza katika kuhakikisha anamaliza kero hiyo katika eneo hilo.

Aidha ametoa vyandarua 300 kwa kina Mama hao ili kuwasidia kujikinga na maradhi ya malaria,ameongeza kuwa ni vyema vyandarua hivyo vikatumika katika matumizi yaliyokusudiwa na sio kwenda kufanyia kazi tofauti.

Mbunge huyo amewaomba wakina Mama hao kuzungumza na vijana wao ili kujitokeza na kutumia fursa zilizopo katika taasisi za kifedha ili kujikwamua kiuchumi.


0 maoni:

Chapisha Maoni