on August 7.2016
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akisalimiana na
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC)
Padre Raymond Saba (kushoto) wakati wa maadhimisho ya siku ya Upashanaji
Habari Kanisani jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Baraza hilo Bw. Bernard James.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akielezea jambo
mara baada ya kutia saini katika kitabu cha wageni ofisini kwa Katibu
Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Padre
Raymond Sabas (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya 50 ya Upashanaji
Habari Kanisani jana Jijini Dar es Salaam. Kulia Mwenyekiti wa Bodi ya
Tumaini Media Padre Joseph Matumaini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akisisitiza
jambo alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya 50 ya Upashanaji
Habari iliyofanyika katika ukumbu wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa
Kanisa Katoliki jana Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu
wa TEC Padre Raymond Saba, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya TEC
Bw. Bernard James na Mwenyekiti wa Bodi ya Tumaini Media Padre Joseph
Matumaini.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya
Mawasiliano TEC Bw. Bernard James akifafanua jambo wakati wa maadhimisho
ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi
za Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) jana Jijini Dar es
Salaam. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa TEC Padre Raymond Saba, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante
Ole Gabriel na Mwenyekiti wa Bodi ya Tumaini Media Padre Joseph
Matumaini.
Katibu Mkuu wa TEC Padre Raymond
Saba akifafanua jambo wakati wa maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari
Kanisani iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa
Kanisa Katoliki jana Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Katibu Mkuu
wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole
Gabriel, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya MawasilianoTEC Bw. Bernard James na
Mwenyekiti wa Bodi ya Tumaini Media Padre Joseph Matumaini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akisalimiana na
Mke wa Waziri Mkuu mstaafu Mama Regina Lowassa wakati wa maadhimisho ya
50 ya Upashanaji Habari Kanisani iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za
Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki jana Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Tumaini
Media Padre Joseph Matumaini akifafanua jambo alipokuwa akiwasilisha
ujumbe wa Baba Mtakatifu Papa Fransisko kuhusu maadhimisho ya 5O ya siku
ya Mawasiliano duniani jana Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Elimu wa
Jumuiya za Kikristo (CSSC) Bw. Petro Pamba akielezea jambo alipokuwa
akiwasilisha mada kuhusu changamoto za mawasiliano katika uinjilishaji
mpya wakati wa maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani leo
Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki katika
maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani yaliyofanyika katika
ukumbi wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC)
wakifuatilia mada zilizowasilishwa katika maadhimisho hayo jana Jijini
Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki katika
maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani yaliyofanyika katika
ukumbi wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC)
wakichangia mada jana Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa TEC Padre Raymond
Saba akisalimiana na Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Regina Lowassa
wakati wa maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani iliyofanyika
katika ukumbi wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki jana
Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na: Frank Shija, MAELEZO.
…………………………………………………………………………………….
Na Shamimu Nyaki-WHUSM
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel amewataka
wanahabari nchini kuandika na kuripoti habari kwa jamii ambazo zina
ukweli na zinazotoa elimu kwa jamii kuhusu maendeleo.
Prof. elisante Ole Gabriel
ameyasema hayo wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Upashanaji
Habari Kanisani yaliyofanyika jana Kurasini Jijini Dar es Salam ambapo
amesema wanahabari nchini wanapaswa kutumia vyema taaluma yao na maadili
ya uandishi wa habari.
Aidha Katibu Mkuu huyo amesema
kuwa ni vyema wanahabari kwenda na mabadiliko ya teknolojia kwa kuitumia
vizuri katika masuala ya kutoa habari kwa jamii bila kuathiri
Utamaduni na amani iliyopo nchini.
“Kuweni makini katika matumizi ya
teknolojia katika kile mnachotaka kuandika ili mlinde Utamaduni
wetu,yale yanayokwenda kwa jamii muyachuje na lazima muyajue vizuri na
kwa usahihi ili kuepuka matokeo hasi kwa jamii”.Alisema Prof.Elisante
Ole Gabriel.
Kwa upande wake Padri Joseph
Matuamaini ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tumaini Media amesema kuwa
vyombo vya habari lazima viwe na Sera na Dira ambayo inaeleweka kwa
watazamaji ili iwe rahisi kuelewa ujumbe wanaoufikisha.
“Vyombo vya habari vya kidini
kuweni na huruma kama Baba wa Mbinguni ,lazima mufikishe ujumbe kwa
jamii kuhusu Utukufu wa Mungu na umuhimu wa amani ili kuondoa hofu kwa
wananchi”.Alisema Padri Matumaini.
Padri Mtumaini ameongeza kuwa
vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuelimisha jamii kuhusu umuhimu
wa Serikali kuhamia Dodoma ili kuondoa hofu iliyoingia moyoni mwao kuwa
itadhorotesha maendeleo.
Rais alipotangaza Serikali kuhamia
Dodoma wananchi waliingiwa na hofu,lakini hakuna sababu ya kuogopa bali
tuamini kuwa ni hatua nzuri ya kuleta maendeleo na kutimia kwa ndoto ya
muda mrefu ya Taifa letu.
Maadhimisho hayo yalibeba pia
ujumbe wa Baba Mtakatifu Papa Francis mabao umesisitiza namna bora ya
kutumia mawasiliano katika kutangaza mambo mazuri ya Mungu kwa jamii.
0 maoni:
Chapisha Maoni