SERIKALI
wilayani Sikonge mkoani Tabora,imewaagiza walimu shule za msingi na
sekondari,kutenga muda kwa ajili ya kuwaelimisha (afya ya uzazi)
wanafunzi wa kike juu ya vipindi vya ukuaji wa miili yao, ili kuwajengea
mazingira mazuri ya kujilinda baada ya kufikia kipindi cha kubalehe.
Imedaiwa
kwa njia hiyo,itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza maambukizo ya
magonjwa ya zinaa, na mimba zisizotarajiwa kwa wanafunzi hao.
Agizo
hilo limetolewa na Mkuu wa wilaya ya Sikonge, Peres Boniphace
Magiri,wakati akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya msaada wa
madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni tano, yaliyotolewa na NMB
benki tawi la Sikonge kwa shule ya msingi Kiyombo.
Alisema
miili ya binadamu na hususani ya watoto wa kike, inabadilika kadri ya
miaka inavyozidi kusonga mbele, ambapo inafika wakati msichana ana
balehe na kuanza kupenda vitendo vya ngono.
“Ili
kuepukana na vitendo hivyo, mwanafunzi wa kike anapaswa awe
ameelimishwa mbinu bora za kukabiliana na mihemuko ya aina mbalimbali
inayochochea kufanya ngono.Pia waelemishwe juu ya madhara yanayoweza
kusababishwa na vitendo hivyo”, alisema na kuongeza kwa kusema;
“Mkoa
wa Tabora ni wa kwanza kwa mambo ya ovyovyo yakiwemo ya mimba kwa
wanafunzi na wasichana wenye umri chini ya miaka 18,kadhalika kwenye
mitihani ya kitaifa ya darasa la saba,umekuwa wa mwisho kwa miaka mitatu
mfululizo.Vile vile ni wa mwisho kwa mambo ya msingi yakiwemo ya
maendeleo ya wananchi wake”.
Mkuu
wa wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, Peres Boniphace Magiri, akizungumza
kwenye hafla ya makabidhiano ya msaada wa madawati 50 yenye thamani ya
shilingi milioni tano yaliyotolewa msaada na NMB tawi la Sikonge.Kulia
ni Meneja NMB tawi la Itigi,Victor Dilunga anayefuata ni Meneja NMB tawi
la Sikonge, Stewart Singo. Wa tatu kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji
halmashauri ya wilaya ya Sikonge,Simon Ngatunga akiteta na diwani wa
kata ya Kiyombo.
Akiijengea
nguvu hoja yake hiyo,Magiri alisema kuwa tatizo la mimba zisizotarajiwa
kwa wanafunzi wa kike wilaya ya Sikonge na mkoa wa Tabora kwa ujumla,ni
kubwa na linachangia kuharibu matarajio ya wanafunzi wa kike kufika
mbali kielimu.
Aidha,Magiri
amewataka walimu wawe mfano kwa kuacha vitendo vya kujihusisha
kimapenzi na wanafunzi wao wa kike.Wakati huo huo,wawachunge mienendo ya
wanafunzi hao wa kike.
Katika
hatua nyingine, Mkuu huyo wa wilaya, alisema mikutano ya hadhara katika
wilaya hiyo ya kuhamasisha wananchi kujiletea maendeleo, itafanywa na
viongozi waliochaguliwa katika maeneo yao tu, na si vingenevyo.
Kwa
upande wake Meneja wa NMB kanda ya magharibi, Leon Ngowi,,alisema NMB
katika mipango yake,imekuwa ikishiriki shughuli mbalimbali za
kijamii,husasani kwenye sekta ya elimu,afya na pia kufariji jamii pindi
wanapopatwa na majanga kama mafuriko na ajali za barabarani.
Meneja
NMB tawi la Sikonge mkoani Tabora, Stewart Singo, akitoa taarifa ya
msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni tano
yaliyotolewa na tawi hilo lwa shule ya msingi ya Kiyombo halmashauri ya
wilaya ya Sikonge mkoani Tabora. Meneja Singo alitoa taarifa hiyo kwa
niaba ya Meneja NMB kanda ya masgharibi,Leon Ngowi. Wa pili kulia
aliyekaa ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge,
Simon Ngatunga.
“Kwa
mwaka huu, NMB imetenga zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya
kuchangia maendeleo ya wananchi kwenye sekta ya elimu na afya. Kiasi
hiki kinatufanya kuwa benki ya kwanza katika kuchangia maendeleo kuliko
benki yoyote nchini.Kwa msaada huu wa madawati,ni sehemu ya benki yetu
kumuunga mkono Rais Magufuli,kutimiza ahadi yake ya elimu bure”,alisema.
Aidha,Meneja
Ngowi ambaye taarifa yake ilitolewa kwa niaba yake na Meneja NMB tawi
la Sikonge,Stewart Singo,ametumia fursa hiyo, kuwahimiza walimu wakuu wa
shule za msingi Bangayegya, Lulanga na wenyeviti wa kamati za
shule,kuhakikisha shule hizo zinapata mafanikio ya hali ya juu kielimu
na hivyo, kuwa mfano bora hapa nchini.
Wakati
huo huo, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge,Simon
Ngatunga,amewataka walimu kutekeleza majukumu yao kikamilifu,ili wawe na
haki ya kudai stahiki zao.
Aidha,Ngatunga
aliahidi kuanzisha utoaji wa tuzo kwa shule zitakazofanya vizuri kwenye
mitihani ya kitaifa,lengo likiwa ni kuchochea maendeleo ya sekta ya
elimu katika halmashauri hiyo.
Na Nathaniel Limu, Sikonge
Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge, Simon Ngatunga,
akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya msaada wa madawati 50 yenye
thamani ya shilingi milioni tano yaliyotolewa na NMB tawi la Sikonge kwa
shule ya msingi Kiyombo. Pamoja na mambo mengine, Ngatunga amewahimiza
walimu kufanya kazi kwa moyo na kujituma, ili waweze kujijengea
mazingira mazuri ya kuendelea kulipwa stahili zao.Wa kwanza kulia ni
Mkuu wa wilaya ya Sikonge, Peres Boniphace Magiri.Kushoto ni wajumbe wa
kamati ya shule pamoja na mjumbe wa kamati ya ulinzi.
Mkuu
wa wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, Peres Boniphace Magiri, akikata
utepe kuathiria makabidhiano ya msaada wa madawati 50 yenye thamani ya
shilingi milioni tano yaliyotolewa msaada na NMB tawi la Sikonge kwa
shule ya msingi ya Kiyombo.
Meneja
NMB tawi la Sikonge mkoani Tabora, Stewart Singo (kulia) akimkabidhi
mkuu wa wilaya ya Sikonge,Peres Boniphace Magiri, madawati 50 yenye
thamani ya shilingi milioni tano yaliyotolewa msaada na benki hiyo kwa
shule ya msingi Kiyombo.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya msingi Kiyombo wilaya ya Sikonge mkoani
Tabora,wakifurahia msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi
milioni tano yaliyotolewa msaada na NMB tawi la Sikonge.(Picha zote na
Nathaniel Limu).






0 maoni:
Chapisha Maoni