Mwenyekiti
wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Mhandisi Steven
Mlote(kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam,wakati wa alipokuwa akitoa tamko la baraza hilo juu ya kuvifutia
Usajili baadhi ya vyuo ambapo kati ya 175 vimepewa notisi ya kushushwa
hadhi na 5 vimefutiwa Usajili na 41 vimetakiwa kujisajili mara moja
,ikiwa katika jitihada za kuboresha elimu ya ufundi nchini,Katikati
Kaimu wa baraza hilo Dkt. Adolf Rutayuga na Mkurugenzi wa
Udhibiti,Ufuatiliaji na Tathimini Bi. Agness Ponera.
Baadhi ya wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
wakiwa kwenye mkutano wakati Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhandis Steven
Mlote(hayupo pichani)alipokuwa akiongea na waandishi habari jijini Dar
es Salaam kuhusiana na tamko la baraza hilo kuvifutia Usajili baadhi ya
vyuo ambapo kati hivyo 175 vimepewa notisi ya kushushwa hadhi na 5
vimefutiwa Usajili na 41 vimetakiwa kujisajili mara moja,ikiwa katika
jitihada za kuboresha elimu ya ufundi nchini.
………………………………………………………………………………………………………
Baraza la Taifa la Elimu ya
Ufundi (NACTE) limetangaza kuwa vyuo 5 vimefungwa kuendesha mafunzo na
kufutwa kwenye rejista ya vyuo vya ufundi nchini.
Pia Baraza limetangaza kuwa vyuo
41 vinavyotoa elimu ya ufundi bila kusajiliwa kwa mujibu wa sheria
vimepewa muda wa wiki mbili na kutakiwa vijisajili mara moja kwenye
Baraza hilo kabla ya kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Vilevile, vibali vya usajili wa
vyuo 112 vya kutoa elimu ya ufundi vimefikia ukomo hivyo vinapaswa
kutekeleza masharti ya Usajili; wakati vyuo 57 vimefikia ukomo wa
ithibati, hivyo inapaswa kutekeleza masharti ya ithibati, imetangazwa
jana.
Akiongea katika mkutano na
waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Baraza (NACTE), Mhandisi Steven
Mlote, amesema Baraza limetoa muda wa mwezi mmoja kwa vyuo 112
kutekeleza masharti ya usajili na vyuo 52 kutekeleza masharti ya
ithibati kwa mujibu wa sheria za uendeshaji vyuo vya ufundi nchini, na
vyuo vitakavyoshindwa kutekeleza agizo hili vitafungiwa mara moja.
Mhandisi Mlote pia alitoa onyo
akisema “vyuo 41 vinavyotoa elimu ya ufundi bila kusajiliwa kwa mujibu
wa sheria nimevipa muda wa wiki mbili na navitaka vijisajili mara moja
kwenye Baraza kabla ya kuchukuliwa hatua kali za kisheria”.
Mhandisi Mlote alivitaja vyuo vyote vyenye matatizo kama ifuatavyo:
Jedwali I: Vyuo vya Ufundi Vilivyofutiwa Usajili
NA. | CHUO |
State College of Health and Allied Sciences – Dar es Salaam | |
Zoom Polytechnic College – Dar es Salaam | |
Tabitha College – Dar es Salaam (formerly: Thabita Vocational Training College – Dar es Salaam) | |
Financial Training Centre – Dar es Salaam | |
TMBI College of Business and Finance – Dar es Salaam |
Jedwali II: Vyuo ambavyo Havijasajiliwa na vinavyoendesha Programu zisizo na Kibali cha Baraza
NA. | CHUO |
1. | King Solomoni College – Arusha |
2. | Avocet College of Hotel Management – Arusha |
3. | Kewovac Nursing Training Centre – Mbagala, Dar es Salaam |
4. | St. Family Health Training Institute – Mbagala, Dar es Salaam |
5. | Bethesda Montessori Teachers Training College – Arusha |
6. | Green Themi Teacher’s College & Green Themi Institute of Tourism |
7. | Mainland Institute of Professionals – Arusha |
8. | St. David College of Health – Dar es Salaam |
9. | Islamic Culture School – Dar es Salaam |
10. | Tanzania Education College – Dar es Salaam |
11. | Macmillan Training College – Dar es Salaam |
12. | Tanzania International University (TIU) – Dar es Salaam |
13. | Dodoma College of Business Management – Dodoma |
14. | Faraja Health and Emergencies – Mbeya |
15. | St. Joseph College – Mbeya |
16. | St. Peter Health Management – Mbeya |
17. | Kapombe Nursing School – Mbeya |
18. | Uyole Health Institute – Mbeya |
19. | Josephine Health Institute – Mbeya |
20. | Institute of Public Administration – Chake chake Pemba |
21. | Dar es Salaam College of Hotel and Business Studies – Vuga, Unguja, Zanzibar and Chake Chake, Pemba, Zanzibar |
22. | Zanzibar Training Institute, the Professional College of Information Technology, Languages and Business Studies – Mwera Meli Sita Unguja Zanzibar |
23. | Azania College of Management – Raha Leo, Zanzibar |
24. | Time School of Journalism – Chakechake, Pemba |
25. | Residence Professional College – Mombasa, Zanzibar |
26. | Mkolani Foundation Organisation – Mwanza |
27. | Kahama College of Health Sciences – Kahama |
28. | Institute of Adult Education-Mwanza Campus – Luchelele Site |
29. | Zoom Polytechnic – Bukoba |
30. | Johrow Star Training College – Shinyanga |
31. | St. Thomas Training College – Shinyanga |
32. | Dar es Salaam School of Journalism and Mass Communication DMSJ – Bukoba |
33. | Dar es Salaam School of Journalism and Mass Communication (DMSJ – Mwanza |
34. | Dar es Salaam School of Journalism and Mass Communication (DMSJ – Geita |
35. | Dar es Salaam School of Journalism and Mass Communication (DMSJ – Simiyu |
36. | Harvest Institute of Health Sciences – Mwanza |
37. | Singin International – Bukoba |
38. | College of Business Management – Mombasa, Zanzibar |
39. | Tanzania Star Teachers College – Chakechake, Pemba, Zanzibar |
40. | Tanzania Star Teachers College – Unguja, Zanzibar |
41. | St. Mary’s International School of Business – Sumbawang |
0 maoni:
Chapisha Maoni