Alhamisi, 11 Agosti 2016

Uharibifu wa Vifaa vya Kuhifadhia Taka Vituo vya Mabasi ya Mwendo Kasi Vipi..??


Hapa upande wa kulia ukionekana kuwa kifaa cha kuhifadhia taka kilisha chomolewa na kubakiza mfuniko tuu na papo hivi kwa zaidi ya mwezi sasa.

Hapa Kifaa cha kuhifadhia taka taka kikiwa kimepinda haijulikani kiligongwa au kuna watu walikuwa wanataka chomoa.

Hiki kikiwa kimelegea kabisa amambapo muda wowote litachomoka.

Hapa mfuniko ndio ulisha potea tena...

Hili nalo tayari linaelekea kudondoshwa chini.

Hii hapa ndio funga kazi kabisa yani wamesha chomoa muundo mbinu wote wa kushoto 

Picha na Fredy Njeje 
 
Ikiwa ni Takribani miezi michache kupita tangia mabasi ya mwendo kasi yaanze kufanya kazi kwa ufanisi mzuri, kumekuwa na mambo kadha wa kadha yakiendelea ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa miundombinu ya vituo hivyo vya mabasi hayo.

Hili limeonekana bila chenga Morogoro Road ambapo kipande cha kutokea Jangwani mpaka Manzese kikionesha wazi  vifaa vya kuhifadhia taka vimeharibika, huku vingine vikionekana kuchomolewa, kupinda, na kulegea. 

 Swali la kujiuliza hapa ni kwamba kwa jinsi miundombinu hii ilivyo kaa  ni ngumu sana hata mtu kugonga kwa mguu sasa inakuwaje inaharibika kiasi hiki?.

0 maoni:

Chapisha Maoni