Postedy by Esta Malibiche on August 12.2016 in News with No comment
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina
Chuwa akitoa taarifa ya ofisi yake ilivyojipanga katika kusimamia
takwimu za taifa wakati wa uzinduzi wa warsha ya kitaifa kuhusu mpango
wa Takwimu za Malengo ya Milenia kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Mhandisi John Kijazi leo jijini Dar es salaam. Warsha hiyo
inashirikisha wadau wa ndani na nje ya nchi.
……………………………………………………………………………..
Na May Simba na Eleuteri Mangi, MAELEZO
Serikali kupitia Ofisi ya Taifa
ya Takwimu (NBS) imezindua mpango wa kuboresha matumizi ya takwimu
sahihi katika kutekeleza malengo 17 ya dunia kwa maendeleo ya nchi.
Akizungumza na wadau wa takwimu
jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa warsha ya kitaifa kuhusu
mpango wa Takwimu za Malengo ya Milenia kwa niaba ya Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Aziz Mlima amesema kuwa
matumizi ya takwimu sahihi yataisaidia Serikali kutekeleza sera na mingo
ya ili kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
Malengo hayo ni pamoja na
kutokomeza umasikini, njaa, kuimarisha afya na ustawi, Elimu bora, usawa
wa jinsia, maji safi na salama, nishati mbadala kwa gharama nafuu, kazi
zenye staha na ukuzaji uchumi, viwanda, ubunifu na miundombinu, na
jamii endelevu.
‘
Malengo mengine ni matumizi na
uzalishajinwenye uwajibikaji, kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya
tabia nchi, kuendeleza uhai katika maji, kulinda uhai katika ardhi,
amani, haki na taasisi madhubuti pamoja na ushirikiano ili kufanikisha
malengo.
Dkt. Mlima amesema kuwa mpango
huo uliozinduliwa utaisaidia Tanzania kufikia malengo ya maendeleo
endelevu kulingana na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2025.
Aidha, Serikali inaendelea
kusimamia kuwekeza zaidi katika ukusanyaji wa takwimu sahihi kwa lengo
la kuweka, kufuatilia na kutekeleza mipango yake kwa kulingana na
malengo iliyojiwekea.
“Hatua hii itasaidia kuendeleza
malengo ya SDG kupitia upatikanaji wa takwimu kwa njia ya uwazi ambayo
itakuwa ya haraka kutuonyesha mapungufu na hivyo kutatua changamoto
zinazoikabili jamii” Dkt. Mlima
Dkt. Mlima amezitaka Wizara,
Taasisi na Mashirika mbalimbali kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha
uwepo wa usimamizi thabiti katika kupima matarajio ya maendeleo
yanayokusudiwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu
wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa lengo la
warsha hiyo ni kuja na mipango ambayo itahusisha matumizi sahihi ya
takwimu zitakazoisaida Serikali kutatua changamoto zilizopo na kutoa
mwelekeo katika kutekeleza sera za nchi.
Vilevile, Dkt. Albina amesema
kuwa, mpango huo utahusisha wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi
ambapo wamependekeza kuwepo kwa kamati itakayohusisha viongozi wa juu wa
Serikali na kusimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu au Ofisi ya Katibu Mkuu
Kiongozi kwa kuwa wapo kwenye ngazi ya maamuzi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya
Takwimu Afrika Kusini, Bw. Pali Lehohla amesema kuwa Tanzania ni
miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika suala la takwimu na kushauri
mataifa mengine ya Afrika kujifunza namna Ofisi ya Taifa ya Takwimu
inavyopaswa kuongozwa na uongozi bora na imara.
0 maoni:
Chapisha Maoni