Jumapili, 7 Agosti 2016

RAIS DKT. MAGUFULI ASALI KATIKA KANISA LA BIKIRA MARIA PAROKIA YA CHATO, PIA ATEMBELEA KANISA LA ANGLIKANA CHATO, KANISA LA AIC PAMOJA NA MSIKITI WA OMAR BIN-L-KHATTAB CHATO MKOANI GEITA

 Postedy by Esta Malibiche on August 7.2016 in News with No comment
chat1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakisali katika ibada ya Jumapili katika Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
chat2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waamini wa kanisa Katoliki wa Parokia ya Chato mara baada ya Ibada katika kanisa hilo Chato Mkoani Geita.
chat3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihamasisha mchango wa ujenzi wa Kanisa jipya la la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
chat4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Padre wa Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Henry Mulinganisa mara baada ya kushiriki Ibada katika Kanisa hilo.
chat5
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na na Padre wa Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Henry Mulinganisa mara baada ya kuwasili kwenye kanisa hilo.
chat6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono waamini wa Kanisa Katoliki Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita hawapo pichani mara baada ya kushiriki Ibada katika kanisa hilo.
chat7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimsikiliza Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Chato Zacharia Samson mara baada ya kuwasili katika kanisa hilo la Anglikana Chato Mkoani Geita.
chat8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiimba wimbo wa Amani pamoja na Kwaya ya Kanisa la  African Inland Church la Chato Mkoani Geita mara baada ya kuwasili katika kanisa hilo.
chat10 chat11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Mwalimu wake wa zamani wa Shule ya Msingi Chato Mkoani Geita Mwalimu Mkuu Mstaafu  Jackson Nyamwaga mara baada ya kumuona wakati akitoka katika Kanisa la  African Inland Church la Chato Mkoani Geita.
chat12
Shekhe wa Bakwata Wilaya ya Chato Hassan Issa Mnubi akiongoza dua ya Kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli nje ya Msikiti wa Omar Bin-L-Khattb Chato Mkoani Geita.
 PICHA NA IKULU

0 maoni:

Chapisha Maoni