Na Esta Malibiche
Iringa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba ameagiza uongozi wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Iringa
kuanza mara moja mchakato wa kuhamisha Gereza kuu la mkoa kutoka katika mji na
kwenda pembezoni mwa mji.
Gereza hilo lililopo katika kata
ya Miomboni lipo katika kati ya mji na jirani na Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa
Iringa na uwepowake umelalamikiwa na wakazi wa mji huo wanaodai umekuwa
ukiwakwamisha kufikisha wagonjwa hospitalini kutokana na barabara hiyo kufungwa
nyakati za usiku kwa sababu za kiusalama.
Akizungumza mara baada ya
kufanya ziara ya siku moja mkoani hapa na kutembelea eneo hilo kujionea hali
halisi Nchemba aliuagiza uongozi wa gereza kuanza mchakato wa kulihamisha
gereza hilo lililopokata ya Miyomboni Kitanzini na kulipeleka katika katikakata
ya Kwa kilosa lilipogereza dogo la Mlolo.
“Nimekuja baad aya kusikia kuna
malalamiko nikaona nijenitembeleleenione eneolamgogoro ni lipi,nimefika
eneohilonakujionea ni kweli pale pamebanana,gereza ingawaje limejaa kuptiakiasi
hakuna eneo la kufanyiaupanuzi wakati huo huophosptali wanaotakiwakujenga
kitengo cha dharura hawana eneo la kufanyia upanuzi”alisema Nchemba na
kuongeza:
‘Kutokana na sababu hizo na
kwakuwa Gereza wanaeneo pembezeno ambalo ni kubwa na lipo umbali wa km 7
ninaagiza uongozi wa gereza hili la Mkoa kuanza mchakato wa ujenzi wa
Gereza hilojipya kwa kuchambua wafumgwa waliopo kupata idadi ya wale wenyeuwezo
wa kufanya kazi ili watumeke kwenye ujenzi huo”alisema.
Nchemba aliagizo uongozi huo
uchambuziwa wafungwa waliopokatika gereza hilowenye uwezo wa kufanya
kaziufanyike sambamba na kazi ya kubaini vifaa vinavyotakiwa katikakazi ya
kufyatua tofali vikiwamo vibao vya kufyatulia tofali ilikazi ya ujenzi wa
Gereza hiloianze mara moja.
Alisema hatua hiyo pia itasaidia
kuondoa msongamano wa wafungwa waliopo katika gereza la mkoa ambao ni katiya
450 na 500 ilehali gereza hilo linauwezo wa kuhifahdi wafungwa 220 tu jambo
alilodai nimuhimu kulihamishie kwenye eneo la Kwakilosa lenye ukumbwa wa
hekta 325.
Katika hatua nyinjgine Waziri
huyo aliwaeleza wafanyakazi waliopo chini ya Wizara yake ambao ni askari
Magereza,Polisi,Uhamiaji na asakari wa zimamoto kuwa na subira wakati
malalamiko yao yanayohusiana na posho za nyumba,Kuongeza Nyumba za askari na
sare za askari na kwamba serikali itayafanyia kazi.
Awali akitoa taraifa ya Mkoa huo
mbele ya Waziri, Kaimu Mkuu Mkoa wa Iringa Richard Kasesela alisema kuwa
changamoto inayowakabili wakaziwa Iringa ni kufungwa kwa barabara inayokwenda
katika Hosptali ya Rufaa ikipitia eneo la gereza kuu la mkoa.
Alisema kutokana na malalamiko
ya wananchi hao,serikali mkoani hapa imefutalia jambo hilo kwa muda mrefu bila
ya mafanikio.
Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi Iringa Mjini Abed Kiponza alimtaka waziri huyo kuamuru kuondolewa ukuta huo uliojengwa na uongozi wa gereza hilo
uvunjwe ili kuruhusu gari kupitisha wagonjwa katika eneo hilo na wananchi
wanaoenda kuwaangalia wagonjwa waondokane na adha iliyokuwa ikiwakabili.
“Kufungwa kwa barabara hii
kumesababisha matatizomakubwa kwa wananchi wetu tumepoteza maisha yawagonjwa
katiya sitanasababu kutokana na kuchelewa kuwafikisha wagonjwa kwenye
huduma,tunaomba Mheshimiwa Waziri utusaidie katika hili”alisema Kiponza.
mwisho |
0 maoni:
Chapisha Maoni