Jumatano, 10 Agosti 2016

MAKATIBU WAKUU WATEMBELEA KITUO MAHIRI CHA KUTUNZA KUMBUKUMBU (INTERNET DATA CENTRE) KILICHOPO ENEO LA KIJITONYAMA DSM.

Postedy by Esta Malibiche on August 10.2016

TC1
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia sekta ya Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo akitoa maelezo ya kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu (internet Data Centre) kwa Makatibu Wakuu hawapo pichani walipotembelea kituo hicho kilichopo eneo la Kijitonyama DSM.
TC2
Katibu Mkuu wa Wizara  ya  Ardhi Dkt. Yamungu Kayandabila   katikati akitoa   maoni  yake kuhusu  kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu “ internet Data Centre”,  (wa kwanza kulia) ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Mwinyi na (wa kwanza kushoto) ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri walipokitembelea kituo hicho eneo la Kijitonyama DSM.
TC3
Afisa kutoka Kampuni ya Simu Tanzania TTCL Bw. Suleimani Kagobe  akitoa maelezo kwa Makatibu Wakuu jinsi mfumo wa umeme unavyofanya kazi walipotembelea katika kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu kilichopo eneo la Kijitonyama DSM.

0 maoni:

Chapisha Maoni