Jumatano, 10 Agosti 2016

Kuelekea Siku ya Kijana Duniani Vijana Wakutana Kujadili Changamoto Zao

Mwakilishi Mkazi msaidizi kutoka UNFPA Bi. Christine Mwanukuzi akifungua mdahalo huo, kuwashukuru vijana kwa kujumuika pamoja na kuwapongeza kwa kufanikisha mdahalo huo kuelekea katika siku ya vijana duniani siku ya tarehe 12.08.2016.

Bw. Badru Juma Rajabu akielezea historia ya siku ya vijana ilipoanzia na kusisitiza kuwa vijana wanatakiwa kutambulika na wasisahau kuchukua fursa pale wanapowezeshwa.

Oscar Kimario muwezeshaji kutoka Restless Development akielezea baadhi ya ripoti juu ya vijana na kuwasihi vijana kuwa ndio watakuwa mstari wa mbele katika maendeleo endelevu hivyo wanapaswa kujituma na kufanya kazi kwa bidii.

Vijana wakiendelea kufuatilia mdahalo huo kwa makini.

Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa ILO Nancy Lazaro akizungumzia ajira zenye staha ,alisema kuwa vijana wengi wameajiriwa lakini katika ajira zisizo na staha na kusisitiza ifike kipindi sasa vijana waajiliwe na kazi zenye Staha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Msichana Initiatives Rebeca Gyumi akijibu maswali mbalimbali ambayo waliuliza vijana waliofika katika kongamano hilo na kusema kwamba sio kweli kwamba wanafunzi waliomaliza elimu ya vyuo ni vilaza.

Vijana wakiendelea kufuatilia wajibu maswali wakijibu yale waliyo yauliza.

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St.Josephs Veronica Shayo kidato cha tano akisisitiza vijana kuwa na tabia za kuweka akiba kwa kile wanachopata ili kije kuwasaidia pindi watakapo kuwa wakubwa.
Picha ya pamoja ya Baadhi ya Washiriki wa Mdahalo huo.

0 maoni:

Chapisha Maoni