Jumapili, 2 Oktoba 2016

ZIARA YA NAIBU WAZIRI TAMISEMI YAMUINGIZA KIKAANGONI MGANGA MKUU MANISPAA YA KIGOMA

Posted by Esta Malibiche on Octo3.2016 in NEWS with No Comment
Naibu Waziri Suleiman Jafo akikagua mradi  wa Maji katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita
Naibu waziri  ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo amemwagiza katibu Tawala wa mkoa wa Kigoma  kuunda timu ya uchunguzi  juu ya malalamiko  ya wananchi kuhusu tuhuma za wizi wa dawa za serikali katika Hospital  na ubadhirifu wa fedha  za  ujenzi wa wodi ya  kinamama ya katika Zahanati ya  buhanda pamoja  na ujenzi uliofanyika katika zahanati  zilizopo ndani ya manispaa ya kigoma.
 Hatua hiyo imefikiwa baada ya Naibu waziri kutembelea jengo la wazazi la zahanati ya buhanda katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni  ndani ya mikoa Minne kuanzia September 25  hadi 30 ambayo ni Mkoa wa Mara,Simiyu,Geita na kuhitimisha mkoa wa Kigoma,ambapo  alizifikia  Halmashauri 19 ziliziopo ndani ya mikoa hiyo,na kuzungumza na watumishi zaidi ya 600.
Akiwa Mkoani  Kigoma hakuridhishwa kabisa  na utendaji  kazi wa mkuu wa idara ya Afya ya manispaa ya kigoma ndugu John Chacha Maganga kutokana na usimamizi mbovu wa miradi iliyoko katika idara yake sambamba na kuwepo kwa malalamiko mengi ya ubadhirifu wa madawa ndani ya manispaa hiyo.Pia hakuridhika na maelezo ya ujenzi wa jengo la Zahanati  kutoa kwa Mganga mkuu lililojengwa chini ya kiwango ukilinganisha na fedha zilizotolewa na hivyo kusababisha Naibu Waziri kupata  mashaka makubwa kuhusu upotevu wa fedha nyingi katika ujenzi wa jengo hilo lililozinduliwa kinyemela na DMO….
Ziara hiyo  ya siku sita aliifanya baada ya kufunga mkutano mkuu wa  32 wa Jumuiya ya Taasisi za serikali za mitaa[ ALAT ]uliofungwa rasmi tarehe 24.september  2016  mjini Musoma mkoani Mara, huku akikagua miradi 25 ikiwemo miradi ya Barabara,Maji,Afya,Elimu na Ujasiliamali,ambapo ziara yake imeleta tija kwa watumishi wa Halmashauri za wilaya  na wananchi kwa ujumla kuinua hamasa ya utendaji kazi.
 Jafo aliwataka wakurugenzi kuweka malengo ya utekelezaji na wakuu wao  wa idara,na wakuu wa idara kuwekeana malengo na na watendaji wao wa chini wanaowaongoza na kuwasihi wakuu wa idara kutowabagua baadhi ya watumishi pia aliwasihi watendaji wa Halmashauri wabadilike katika utendaji wao.
‘’’’’’’ Lengo la ziara yangu ni  kukagua usimamizi wa shughuli za maendeleo zianazofanywa na  serikali ili kuleta ufanisi katika kuwahudumiana  wananchi ndani ya Halmashauri mbalimbali  zilizopo hapa nchi’’’’’’alisema Waziri Jaffo
MWISHO



Naibu Waziri Suleiman Jafo akiwa na Mbunge  wa Mbogwe Mhe.Silvester  Masele wa kikagua mradi  jenereta la kusukuma katika  wilaya ya Mbogwe mkoani Geita

Naibu waziri Suleiman Jafo akikagua  ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Mara mjini Musoma

Naibu waziri Tamisemi Suleiman Jafo akikaguia kiwanda cha Vijana cha kutengeneza  chaki kilichopo mjini Maswa mkoani Simiyu


Naibu Waziri wa Tamisemi Suleiman Jafo akizungumza na wandishi wa Habari mara baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani Geita

Naibu Waziri Suleiman Jafo akiwa na mtoto wa baba wa Taifa Mdaraka Nyerere pamoja na katibu Tawala mkoa wa Mara Edo Mapunda Nyumbani kwa baba wa Taifa Butiama





0 maoni:

Chapisha Maoni