Posted by Esta Malibiche on Oct6.2016 in MICHEZO
KIKOSI cha Mbeya fc kinatarajia kushuka kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya hapo kesho(Ijumaa) kucheza mchezo mwingine muhimu wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya wageni Stand United kutoka mkoani Shinyanga kikiwa bila nyota wake kadhaa wa safu ya ulinzi.
K wa mujibu wa Ofisa habari, Dismas Ten, maandalizi kuelekea mchezo huo yamekamiliki na City itashuka dimbani ikiendelea kuwakosa nyota wake wawili wa safu ya ulinzi, Haruna Shamte na Sankhani Mkandawile ambao walimua kwenye mchezo wa ugenini dhidi ya JKT Ruvu uliochezwa Mlandizi mkoani Pwani na City kufungwa bao 2-0.
“Kwenye kikosi tunaendelea kuwakosa Haruna na Sankhani, hii ni kwa sababu bado wanauguza majeraha lakini taaraiafa njema ni kuwa mlinzi Rajab Zahir amerejea kikosini kuongeza nguvu baaada ya kushindwa kumaliza dakika 90 za chezo dhidi ya Mwadui kufutia maumivu ya kifungo cha mguu, madaktari wamethibitisha kuwa yuko safi na tayari kwa mchezo wa kesho”, alisema.
Katika Hatua nyingine nahodha wa Mbeya City Fc , Kenny Ally ameipogeza timu ya taifa ya vijana Serengeti Boys kwa hatua nzuri waliyofikia licha ya kushindwa kufuzu kwa michuano ya Afrika baada ya kufungwa bao la dakika za lala salama kwenye mchezo wao wa mwisho huko nchini Congo.
“Kifupi nawapongeza wamefanya kazi kubwa sana, hatua waliyofikia ni ya kujivunia kwa sababu wametegeza mwanga mzuri kwenye mashindan mengine yatakayokuja, hii ni tafasiri kuwa shirikisho letu lilikuwa na nia ya dhati ya kuhaikisha tunafanikiwa kilichotokea ni sehemu ya mchezo wa soka” alisema.
Kenny Ally ambaye alikuwa mmoja wa nyota wa timu ya taifa ya Tanzania waliokwenda nchini Brazil na kutwaa kombe la Copa Coca cola licha ya kutoa pongezi wa shirikisho pia alitoa wito kwa rais Jamal Malinzi kuhakikisha anaitunza vyema timu hii ili ije kuwa timu nzuri ya taifa siku za usoni.
“Nampongeza rais na pia ninatoa wito,kuhakikisha wanaitunza vyema timu hii ili ije kuwa timu bora ya taifa siku zijazo, nakumbuka hali iliyotokea kwetu sisi tuliyoenda Brazil na timu ya vijana wakati huo, baada ya kurudi na kombe, hakuna jambo lolote lililoendelea matokeo yake timu ile ikafa na wachezaji tuliokuwepo kusambaa hovyo hivi sasa kuna ambao wameshaacha soka na wachache tumebaki tunaendelea kucheza”‘ alimaliza
0 maoni:
Chapisha Maoni