Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwasilisha hotuba kuhusu ni
jinsi gani Tanzania imejipanga kukabiliana na tatizo la utapiamlo na
udumavu wa akili kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano,
alipomuwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Jijini
Washington DC, Marekani.
Rais
wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim akimpogeza Waziri wa Fedha na
Mipango Dkt. Philip Mpango, baada ya kuwasilisha hotuba kwa niaba ya
Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo kuhusu
watoto kupata lishe bora wakati wa kuzaliwa na kusisitiza wakinamama
wanyonyeshe watoto ipasavyo ili kuondokana na tatizo kubwa la utapiamlo
ambalo mara nyingi huwakumba watoto wanapokuwa wadogo na kusababisha
kupoteza nguvu kazi ya Taifa, Jijini Washington DC.
Rais
wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim akiwa na Mawaziri wa Fedha wa
Afrika akiwemo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philiph Mpango (wa nne
kutoka kulia), Jijini Washington DC.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, wa kwanza kushoto
akisikiliza kwa makini hotuba ya Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong
Kim, katika mkutano uliowahusisha Mawaziri wa Fedha kutoka nchi kadhaa
duniani kama vile Cameroon, Ethiophia, Senegal na Indonesia ambapo rais
huyo aliwataka mawaziri hao wasimamie rasilimali fedha vizuri hasa
katika suala la kukabiliana na changamoto ya utapiamlo na udumavu wa
akili kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano, mkutano uliofanyika
Jijini Washington DC, Marekani.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akibadilishana
mawazo na baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania nje ukumbi wa mikutano.
0 maoni:
Chapisha Maoni