Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia),
akipata maelezo ya mfumo wa utabiri wa hali ya hewa katika Uwanja wa
Kimataifa wa Songwe (SIA) kutoka kwa Mtaalam wa masuala ya hali ya hewa
uwanjani hapo, Wakati alipokagua uwanja huo mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia),
akipata maelezo kutoka kwa Bw. Baraka Mwambipile kuhusu namna ndege
zinavyoongozwa wakati wa kuruka na kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa
Songwe, Wakati alipokagua uwanja huo mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata
ufafanuzi wa michoro ya ujenzi wa jengo la abiria kutoka kwa Mhandisi wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) wakati alipokagua Uwanja wa Ndege wa
Songwe, Mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA) kuhusu
ujenzi wa jengo la pili la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Songwe,
wakati alipokagua uwanja huo Mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili
kulia) akiendelea na ukaguzi wa jengo la pili la abiria katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Songwe, Mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiendelea na
ukaguzi wa wa Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Songwe , Mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia)
akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa kampuni ya Shapriya Co Ltd
anayejenga jengo la pili la abiria wakati alipokagua uwanja wa kimataifa
wa Songwe, Mkoani Mbeya.
………………………………………………………………………………………………….
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa Serikali haitaendelea na
ujenzi wa jengo la pili la abiria katika uwanja wa ndege wa Songwe
uliopo mkoani Mbeya mpaka tume ya watalamu iliyoundwa kuchunguza ili
kujiridhisha kama utaratibu ulizingatiwa kabla ya kuaza ujenzi huo.
Prof. Mbarawa ametoa kauli
hiyo mara baada ya kukagua jengo hilo linalojengwa na mkandarasi wa
Kampuni ya Db Shapriya ya Tanzania ambapo amesema hadhi ya jengo hilo
hairidhishi hivyo ipo haja ya kujiridhisha kama taratibu zote zilifuatwa
kabla ya ujenzi.
Amebainisha kazi ya tume hiyo ya
wataalamu ni kuhakiki namna utaratibu wa kumpata mkandarasi
ulivyofanywa, gharama halisi za mradi na fedha iliyolipwa kwa mkandarasi
kama inaendana na thamani ya jengo hilo.
“Serikali haiwezi kutoa fedha ya
kumalizia jengo hili kabla ya kujiridhisha ili kuhakikisha fedha
tutakazozitoa zitatumika kulingana na ilivyopangwa na thamani ya fedha
inaendana na jengo lenyewe”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Aidha Waziri Prof. Mbarawa
ameeleza ili kuwa na miundombinu imara na ya kudumu ni lazima
kuhakikisha miradi ya ujenzi wa miundombinu inasimamiwa vizuri na
taratibu za kupata mkandarasi bora zinafuatwa.
“Kutokuwa na miundombinu isiyo
imara ni sababu ya wahusika kuweka mbele maslahi binafsi na siyo ya
Taifa”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa
Pia ameutaka uongozi wa Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuhakikisha makosa yaliyojitokezo
kwenye ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza
hayajirudii katika kiwanja hiki.
Kwa upande wake Meneja wa Uwanja
wa Ndege wa Songwe Bw. Hamisi Amiri amemhakikishia Waziri Mbarawa
kusimamia ujenzi uliobaki kwa kuzingatia taratibu na makubaliano
yaliyowekwa ili jengo hilo lidumu kwa manufaa ya Taifa na Mkoa.
Uwanja wa Songwe ni kiungo muhimu
kwa wananchi wa mikoa ya Katavi, Rukwa, Njombe na Ruvuma na katika
mwaka huu wa fedha umetengewa kiasi cha shilingi bilioni 10 kwa ajili ya
kumalizia ujenzi wa jengo la abiria na taa uwanjani hapo.
0 maoni:
Chapisha Maoni